Kim
Poulsen ameteuliwa kuwa kocha mpya wa timu ya Taifa ya mpira wa miguu
ya Tanzania (Taifa Stars) kuanzia Mei 11 mwaka huu kuziba nafasi ya Jan
Poulsen.
Akizungumza
na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, Rais wa TFF, Leodegar Tenga
amesema Kim amepewa mkataba wa mwaka mmoja baada ya Shirikisho kuamua
kutomuongezea mkataba Jan. Mkataba wa Jan uliokuwa wa miaka miwili
unamalizika Julai 30 mwaka huu.
Amesema
kwa vile Taifa Stars inakabiliwa na mechi za mchujo za Kombe la Dunia
raundi ya pili Kanda ya Afrika na mechi za mchujo za Kombe la Mataifa ya
Afrika (CAN), TFF imeona ni lazima iwe na kocha mpya mapema kabla ya
mkataba wa Jan kumalizika.
Kim
ambaye ni raia wa Denmark amekuwa nchini kwa mwaka mmoja sasa
akifundisha timu za Taifa za vijana wenye umri chini ya miaka 17
(Serengeti Boys) na miaka 20 (Ngorongoro Heroes), hivyo anawafahamu
vizuri wa wachezaji wa Tanzania.
TFF
imeanza mchakato wa kutafuta kocha mwingine wa timu za vijana
atakayeziba nafasi ya Kim. Ili kuwa na makocha wenye falsafa moja, kocha
huyo anatafutwa kutoka Denmark.
Naye
Kim ambaye Jumatatu (Mei 14 mwaka huu) atatangaza kikosi cha Taifa
Stars ambacho Juni 2 mwaka huu kuivaa Ivory Coast katika mechi ya
mashindano amesema yuko tayari kwa kazi hiyo na kusisitiza kuwepo
ushirikiano kutoka kwa wadau mbalimbali ili timu hiyo iweze kufanya
vizuri.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)