Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akimkabidhi Wegson Frakson
kiongozi wa kikundi cha waendesha pikipiki cha Soko Kuu Mandela vizibao
maalum vya usalama barabarani kwa ajili ya waendesha bodaboda Mkoani
Rukwa leo, vizibao hivyo vimetolewa na mfuko wa bima ya afya nchini NHIF
kwa vikundi tofauti 15 vya waendesha pikipiki katika Manispaa ya
Sumbawanga. Katikati ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko Ndugu Hamis
Mdee.Vizibao hivyo vinaakisi mwanga utakaosaidia dereva wa bodaboda
kuonekana kirahisi awapo barabarani hivyo huepusha uwezekano wa kupata ajali.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa aliamua kupanda Pikipiki na kujitambulisha kama mmoja
wa wadau wa bodaboda na kusema kuwa anatambua mchango wao katika sekta
ya usafiri nchini haswa kwa watu wa kipato cha chini. Alitumia mwanya
huo kuwaelezea umuhimu wa wao kujiunga na mfuko wa bima ya afya ambapo
walionekana kuhamasika na kuahidi kujiunga na mfuko huo mapema
iwezekanavyo.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akihamasisha waendesha
pikipiki katika Manispaa ya Sumbawanga kujiunga na mfuko wa bima ya afya
leo katika viwanja vya shule ya sekondari Msakila. Alisema kuwa
waendesha bodaboda wanakabiliwa na changamoto kubwa ya ajali za
barabarani jambo lililosukuma kupewa vizibao hivyo maalum
vitakavyosaidia kuonekana kirahisi wawapo barabarani, aliwasihi kujiunga
na mfuko huo kujihakikishia usalama wa afya zao pindi wapatapo matatizo
ya ajali au maradhi ya kawaida.
Kuonyesha
kuwa wamehamasika madereva hao wa bodaboda waliamua kumsindikiza Mkuu
huyo wa Mkoa wa Rukwa hadi ofisini kwake katika umbali
usiopungua kilomita 5 kutoka eneo la tukio. Mkuu wa Mkoa wa Rukwa
alihamasika na kuamua kupiga nao picha ya pamoja kama inavyoonekana
wakiwemo pia viongozi waandamizi wa mfuko wa bima ya afya nchini na
viongozi wa usalama barabarani mkoani Rukwa.
Wazee
wa bodaboda wakiwa tayari wameshavalia vizibao vyenye kuakisi mwanga
(reflector) vilivyotolewa na mfuko wa bima ya afya nchini
vitakavyowasaidia kwenye usalama barabarani.Picha na rukwareview.blogspot.com
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)