Washiriki wa Miss Arusha City Center 2012 wakiwa katika picha ya pamoja tayari kwa kuchuana vikali usiku wa leo
Washiriki
wa kitongoji Kanda ya kaskazini,Miss Arusha City Center 2012, wakiwa
katika picha ya pamoja,safi kabisa tayari kwa kuchuana vikali usiku wa
jumamosi Mei 5 2012 ndani ya hoteli ya Kitalii,Naura Springs Hotel
iliyopo kati kati ya jiji la Arusha.Shindano hilo kiingilio chake
kimepangwa kuwa ni kwa viti maalum ni sh.25,000/= na kwa viti vya
kawaida ni sh 15,000/=
Mashindano
ya Ulimbwende ngazi ya kitongoji Kanda ya kaskazini,Miss Arusha City
Center 2012,yanatarajiwa kufika kileleni jumamosi usiku (Mei 5 ) ndani
ya hoteli ya Kitalii,Naura Springs Hotel iliyopo kati kati ya jiji la
Arusha
Akizungumza
leo asubuhi jijini Arusha,Mratibu wa shindano hilo Bi Upendo Simwita
kutoka kampuni ya Tour Visual Entertainment ambao ndio waandaji wa
shindano hilo,amebainisha kuwa kila kitu kiko sawa na maandalizi
yamekamilika,tayari kwa kumpata mshindi wa MISS REDD’S ARUSHA CITY
CENTRE 2012 usiku wa jumamosi kati wa Walimbwende 20 watakaoshiriki.
Bi
Upendo Simwita amesema kuwa Warembo wote wenye mvuto na wenye vigezo
stahiki wako tayari kwa shughuli moja tu usiku wa jumamosi,anaongeza
kuwa warembo hao wana ari kubwa ya ushindani,na kwamba kuna uwezekano
mkubwa muwakilishi wa Miss Tanzania 2012 akatokea kwenye kitongoji
hicho.
“Shindano
hilo litakalokuwa la tofauti kubwa na miaka ya nyuma litawakutanisha
walimbwende wapatao 20,ambao watachuana vikali jukwaani, na hatimaye
kumpata Mshindi wa Miss Arusha City Center”,alisema Upendo.
Amesema kuwa
kiingilia katika shindano hilo kimepangwa kuwa ni kwa viti Maalum sh
25,000/= na kwa viti vya kawaida sh.15,000/=. Fanya booking yako ya
tiketi mapema kupitia namba – 0755975454 au 0713681059.
Kwa
upande wa Burudani,Upendo amesema kuwa kutakuwepo na Msanii mahiri wa
Muziki wa kizazi kipya aitwaye Sam wa Ukweli,Muziki wa Asili,Live Band
ya Watoto wa Simba pamoja na burudani nyingine mbalimbali
zitakazotolewa na walimbwende wenyewe siku hiyo.
Upendo
amewataja wadhamini wa shindano hilo kuwa ni REDD’S ORIGINAL,NAURA
SPRINGS HOTEL,CLAUDS FM / CLAUDS TV AND MAWINGU CLUB – ARUSHA,BG
HORIZON, MODERN DRIVING SCHOOL,MAKO ADVENTURE,SEBE&BEKI FOR LIFE, MWANDAGO
INVESTMENT,S.G. RESORT,MEJA LINK LTD,GEO SECURITY,GOLDEN ROSE
HOTEL,RIVERSIDE SHUTTLE SERVICES,ARUSHA TRAVEL LODGE,LITTLE ROSES, LA BELLA VISTA,WAKIPAMBWA NA JANETH BEAUTY PAURLOR NA BI. HADIJA HASSAN.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)