Maharusi,Bw.Oltesh
Eliguard Metili na Ssanyu Sylvia Nyinondi wakiaga watu mbalimbali
waliofika ndani ya kanisa la Azania Front,mara baada ya kufunga ndoa
takatifu,mapema leo mchana jijini Dar.
Maharusi
wakiwa na nyuso za furaha mara baada ya kufunga ndoa na kuwa mwili
mmoja mapema leo ndani ya kanisa la Azania Front,jijini Dar.
Maharusi
wakilishana kiapo cha ndoa mbele ya umati mkubwa (haupo pichani)
uliofika kanisani hapo mapema leo mchana kuishuhudia ndoa hiyo ya Bw.Oltesh Eliguard Metili na Ssanyu Sylvia Nyinondi,iliyofanyika ndani ya kanisa la Azania Front.
Mkuu
wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Dk Alex
Malasusa akizibariki pete za ndoa za maharusi kabla ya maharusi hao
kuvishana.
Baadhi ya Wanakwaya kutoka mkoani Arusha wakiimba
Umati wa watu uliofika kuishuhudia ndoa ya Bw.Oltesh Eliguard Metili na Ssanyu Sylvia Nyinondi iliyofanyika mapema leo mchana ndani ya kanisa la Azania Front,jijini Dar.
Maharusi
wakiingia ndani ya kanisa la Azania Front mapema leo mchana,tayari kwa
kufunga ndoa takatifu,pichani shoto ni Waziri Mkuu aliyejiuzulu,Mh
Edward Lowassa na Mkewe, Mama Regina Lowassa wakishuhudia pia tukio hilo
adhimu na la kihistoria kwa Wanandoa.
Maharusi Bw.Oltesh
Eliguard Metili na Ssanyu Sylvia Nyinondi wakiwa na wapambe wao
wakielekea kanisani,tayari kwa kufunga ndoa takatifu,mapema leo mchana.Picha na Michuzijr Blog.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)