BAADA
ya kutamba na wimbo wake wa Nai Nai Msanii anaekuja juu kwa kasi na mshindi wa
Tuzo mbili za Kili Music Award 2012, Omy Dimpoz anataraji kuzindua Single yake
mpya ya Baadae katika ukumbi wa Club
Bilcanas jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
na mtandao huu wa Kijamii, Meneja wa Msanii huyo, Mbaruku Issa ‘Mubenga’
alisema kuwa maandalizi yote yamekamilika na show itakuwa ya uhakika nay a kuvutia.
Mubenga
amesema Ommy Dimpozy anataraji kuzindua wimbo huo aliofanyiwa kazi na Mwandaaji
wa muziki Man Water huku spoting ya wimbo huo ikifanywa na mwanadada Angel.
Aidha
Mubenga amesema Dimpoz atasindikizwa na wakali wa Bongo Fleva, Diamond, Ben Pol
pamoja na msanii Alawi Jr pamoja na Ma DJ wakali wa Bongo kutoka kundi la Super
Deejayz.
Tayari
Dimpoz ameshaanza kuwasikilizisha wimbo huo baadi ya mashabiki wake wa mikoa ya
Mwanza na Moshi wakati wa Ziara ya Wakali wa Kili Music Awartd 2012
inayoendelea ambapo leo atakuwa Mbeya chini ya Bia ya Kilimanjaro.
“Wimbo
ni mkali na mashabiki wanaukubali vilivyo na tunaomba mashabiki wa Bongo Fleva make
tayari kwa singo hiyo mpya itakayoanza sasa kuchezwa katika vituo vya redio na
kumbi za burudani nchini kote baada ya uzinduzi huo,” alisema Mubenga.
Mungenga
amewakata wakazi wa jiji la Dar es Salaam ambao ni mashabiki na wapenzi wa
muziki wa kizazi kipya kujitokeza kwa wingi kumpa support Dimpoz katika
uzinduzi huo wa aina yake katika Club ya Bilcanaz katikati ya jiji la Dar es
Salaam jumapili.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)