Mbunge Tundu Lissu akihutubia mkutano viwanja vya stendi ya zamani mjini Singida, tangu mahakama kuu impe ushindi dhidi ya kesi
Mbunge wa Singida
mashariki(CHADEMA)Tundu Lissu akimtolea mfano muuza maji mjini Singida
kwa kutumia toroli, maarufu kwa jina la 'Chai
Mbunge
wa Singida mashariki(CHADEMA) Tundu Lissu(wa pili kulia),akiingia kwenye viwanja
wa stendi ya zamani mjini Singida kwa ajili ya mkutano
Wafuasi na wapenzi wa CHADEMA wakiitikia kukunja ngumi juu kuonyesh nguvu ya umma katika mkutano huo, mbele ni mtoto Hilda Jack
---
Na Elisante John Aprili 30,2012.
CHAMA
cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimetoa wito kwa viongozi na
wanachama ‘safi’, walio ndani ya CCM, wajiunge mapema na CHADEMA ili
waikomboe nchi, kutoka kwa wezi na mafisadi wa fedha za umma.
Mnadhimu
mkuu, kambi ya upinzani bungeni, Tundu Lissu, alitoa rai hiyo kwenye
mkutano wa hadhara, aliufanya eneo la stendi ya zamani, mjini Singida,
kwa lengo la kukiimarisha chama, bada ya kushinda kesi yake ya uchaguzi.
Lissu
ambaye pia ni mbunge Singida mashariki, aliwashauri wajiondoe mapema,
badala ya kung’ang’ania huko, kusubiri CHADEMA itawale nchi, halafu
ndio wajitokeze kusema na wao ni wafuasi wa chama hicho.
Pia aliwaomba
viongozi, wanachama na wafuasi wa CHADEMA hivi sasa wachukue
tahadhari, vinginevyo watapata madhara makubwa, ikiwemo hata kupoteza
maisha yao.
Alisema
kitendo cha kuuawa kwa mwenyekiti wao huko Usa river, mkoani Arusha na
kukatwa katwa kwa panga wabunge wa CHADEMA mkoani Mwanza, ni onyo kwa
wanachama na viongozi wa chama hicho.
“Vita
hii ni kubwa, lazima tuielewe, kuanzia sasa kaeni chonjo, vinginevyo
CHADEMA tutauawa, mwenyekiti wetu kule Arusha amechinjwa na wabunge wetu
huko Mwanza wamekatwa katwa mapanga, tena mbele ya polisi….tuangalie
sana,”alitahadharisha Lissu.
Kuhusu
ushindi wa kesi iliyomkabili, ambayo ni moja ya mashauri 14
yaliyofunguliwa, kati ya majimbo 23 ya CHADEMA nchini, Lissu aliishukuru
mahakama kumuona hana hatia, ingawa anaamini wadai wamepoteza fedha
nyingi, zinazofikia zaidi ya Sh. Milioni 200, ili ubunge wake
utenguliwe.
Huo
ulikuwa mkutano wa kwanza kufanyika Singida mjini na watatu kimkoa,
tangu mahakama kuu, kanda ya Dodoma, kupitia Jaji Moses Mzuna wa Moshi,
Mkoani Kilimanjaro, kufutilia mbali shauri la kupinga ubunge,
alilofunguliwa na wanachama wawili wa CCM.
Na Elisante John
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)