Kikosi
kamili cha timu ya waTanzania DMV wakiwa na mdhamini mpya wa timu hiyo
Mbunifu wa mitindo ya Kwetu Missy Temeke, akiwana na shabiki Didi Vava,
katika uwanja wa Greencastle, uliopo Burtonsville, Maryland.Tanzania
DMV leo hii iliweza kutinga tena uwanjani kucheza mchezo wake wapili
na timu ya Ethiopia, hadi mpira kumalizika timu hizo zimetoma 0-0 katika
mpango mzima wa ligi ya 2011 Diaspora World Cup zinazoendelea katika
viwanja vya Hyattsville na Germantown jijini Maryland Nchini Marekani.
Mchezaji
wa timu ya Ethiopian akipambana vikali na Yousouf Godson Liuzinho,
kipindi cha kwanza katika ligi ya 2011 Diaspora World Cupkwenye kiwanja
cha Greencastle, kiliopo Burtonsville, Maryland.
Wachezaji wa wa timu ya Ethiopia wakiwania Freekick katika dakika ya 62 ya mchezo huo
Benchi ya Timu ya waTanzania DMV wakiwa wanangalia jinsi ya mchezo huo ulivyokwenda dhiti ya timu ya waEthiopia.
Mchezaji
wa timu ya Ehiopian akijaribu kumpita beki wa timu ya Tanzania,
Emanuel Oumogbao katika mchezo wa pili wa ligi ya 2011 Diaspora World
Cup kwenye kiwanja cha Greencastle, kiliopo Burtonsville, Maryland.
Jukwa
la mashabiki wa timu ya Watanzania DMV, wanne kutoka kushoto akiwa Rais
wa Jumuiya ya Watanzania DMV pia alihudhuria katika mpambano huo.
Didi
Vava, kushoto akiwa na Sharif Qullatein, Dogo Hudhaifa Shatry, na
Mmiliki wa blog ya swahilivilla Abou Shatry, wakiwa katika jukwa la
wapenzi wa timi ya waTanzania DMV.
Mdhamini
mpya wa timu ya waTanzania DMV ambae ni mwana mitindo na mbunifu wa
mitindo ya (Kwetu Fashion Design) Missy Tetemeke akiwa kwenye mpango
mzima wa kuangalia na kuiunga mkono Timu ya Watanzania DMV, (Picha ya
Kulia) Dogo Hudhaifa Shatry akisikiliza kelele za mashabiki wa timu
hiyo.
Mdhamini
wa timu ya waTanzania DMV ambae ni mwana mitindo na mbunifu wa mitindo
ya Kwetu Fashion Design, Missy Tetemeke akiwa na Bendera ya Taifa.
Benchi
la timu ya waEthiopia wakiwa kama mtu nane njee na ndicho kilicho
wasaidia kutoka bila kufungana na Timu ya waTanzania DMV. Picha na habari kutoka kwa mwana blog wetu Abou Shatry wa http://swahilivilla.blogspot.com/
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)