Bw.
Martin Sospeter katikati akilalamikia shutuma zilizoelekezwa kwake na
bendi ya African Stars wakati alipoongea na wanahabari asubuhi hii
kwenye ukumbi wa Busness Kijitonyama, kulia ni Kaimu Meneja wa bendi
hiyo King Dodoo na kushoto ni Rais wa Bendi ya Mashujaa Charles Baba.
Juzi usiku nilishangazwa na kauli ya mkurugenzi wangu wa Asha Baraka
katika vyombo mbalimbali vya habari kuwa amenifukuza kazi kutokana
kuhujumu bendi ikiwemo kushawishi wanamuziki kujiunga na bendi ya
Mashujaa
Kwa kweli kauli ile ilinisikitisha sana kutokana na ukweli kwamba Asha
nilimchukulia kama zaidi ya dada kwani nilifanya naye kazi kwa miaka
14 iweje hii leo aje anitolee maneno ya kunichafua katika vyombo vya
habari?
Mimi sijawahi kuhusika na mpango wowote wa wasanii wa Twanga kuhamia
Mashujaa na wala sikuwa nafahamu mpango huo zaidi ya mwisho wa siku
kusikia fununu za chinichini na mwishowe wasanii hao kutanghazwa
kuhamia Mashujaa.
Leo napenda nitangaze rasmi kwamba nimeachana na African Stars na
kujunga na Mashujaa Entertainment na tayari nimeshasaini mktaba wa kazi
katika bendi hii.
“Nilipanga nifanye taratibu za kumuaga kutokana na kuwa nilikuwa
nafanya kazi kwake bila ya mkataba lakini nimepata bendi hii ambayo
tulikaa na kukubaliana mambo mbal;imbali.
Mbali na mkataba baadhi ya makubaliano na uongozi wa mashujaa ni pamoja
na kunipangia nyumba hali itakayonilazimu kuhama ile iliyokuwa chini ya
Twanga.
Ninaamini nitafanya vema kazi yangu hii mpya kama ilivyokuwa Twanga
ambapo nilidumu kwa muda mrefu na kuchangia kufika hadi hapo
nilipoachia, hivyo naomba ushirikiano kwa uongozi, wanamuziki, Wadau na
hata ninyi mwaandishi wa habari.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)