Mkurugenzi Mtendaji wa New Habari Bw. Hussein Bashe akitoa heshima
zake za mwisho mbele ya mwili wa marehemu Rachel Mwiligwa ulioagwa leo
katika kanisa la Anglican usharika wa Ubungo na kuhudhuriwa na
wanahabari kutoka vyombo mbalimbali vya habari, Marehemu Rachel Mwiligwa
alifariki usiku wa kuamkia Ijumaa iliyopita na anazikwa leo huko Goba
jijini Dar es salaam.
Geneza la mwili wa marehemu Rachel Mwiligwa likiwa kanisani leo wakati wa ibada ya mazishi.
Mmoja wa wahariri wa habari za michezo New Habari Bw. Isiji akilia kwa
uchungu wakati alipotoa heshima zake za mwisho kwa marehemu.
Mkurugenzi wa Radio One Deo Rweyunga akiaga mwili wa marehemu Rachel
huku akiwa ameongozana na Mwandishi wa Makamu wa Rais Boniface Makene.
Mbunge wa jimbo la Ubungo John Mnyika akitoa heshima zake kwa marehemu
huku akiwa ameongozana na Mbunge wa jimbo la Kinondoni Idd Azan.
Mwandishi Grace Hoka akilia kwa uchungu.
Mwimbaji wa bendi ya Extra Bongo Rogati Hega akitoa heshima za mwisho.
Mwanamasumbwi Japhet Kaseba alikuwa ni miongozi mwa waombolezaji walioaga mwili wa marehemu.
Kutoka kushoto ni Said Mwishehe, Bw. Kihampa na Ali Mkongwe wakitoa heshima zao za mwisho.
Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Radio Times Rehure Nyaulawa, Rashid
Kejo na Shafii Dauda wakitoa heshimza zao za mwisho kwa marehemu.
Ndugu na jamaa wa marehemu wakipita mbele ya jeneza la mwili wa marehemu Rachel Mwiligwa.
Debora Kajolo na Saleh Ally wakiaga.
Frolian Kaijage na Amir Muhando wakitoa heshimza zao za mwisho.
Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Radio Times Rehure Nyaulawa akizungumza
na mbunge wa jimbo la Ubungo Mh. John Mnyika mara baada ya kutoa heshima
za mwisho kwa mwili wa marehemu Rachel Mwiligwa.
Geneza la Mwili
wa Marehemu Rachel Mwiligwa likiingizwa kwenye gari maalum tayari kwa
kuelekea huko Goba ambako marehemu atapumzishwa katika nyumba yake ya
milele.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)