Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma
hotuba yake wakati akizindua rasmi Jukwaa la Uchumi wa Kijani, litakaloendelea
kwa siku tatu Mkoani Iringa. Uzinduzi huo umefanyika leo, katika
Ukumbi wa Shule ya Msingi Mtakatifu Dominic Savio, mkoani Iringa.
Naibu
Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, (wa pili kushoto) Eng. Ngosi C.
Mwihava, akiwa ukumbini hapo wakati wa uzinduzi wa Jukwaa la Kijani.
Sehemu ya wadau waliohudhuria uzinduzi huo.
Makamu
wa Rais, Dkt. Bilal, akipokea zawadi kutoka kwa mmoja wa wafanyakazi wa
Taasisi ya Uongozi, Linda Manu, wakati wa hafla ya uzinduzi huo leo.
Msanii
wa Muziki wa Asili na Mashahiri, Mrisho Mpoto, akighani maneno yake yenye
ujumbe Kuhusu Utunzaji wa Mazingira, mbele ya mgeni rasmi Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati wa uzinduzi
wa Jukwaa la Uchumi wa Kijani, uliofanyika Mkoani Iringa leo.
Mrisho Mpoto (kulia) na mwimbaji wa bendi yake ya Mjomba Band, Ismail, wakiimba mbele ya meza kuu wakati wa uzinduzi huo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Taasisi ya Uongozi, baada ya
kuzindua rasmi Jukwaa la Uchumi wa Kijani, mkoani Iringa leo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akipanda mti wa kumbukumbu katika eneo la Shule ya Msingi Mtakatifu Dominic
Savio, baada ya kuzindua rasmi Jukwaa la Uchumi wa Kijani, Leo.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)