Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
na Balozi wa Korea Kusini, Young Hoon Kim, kwa pamoja wakikata utepe
kuzindua rasmi chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi cha VETA kilichojengwa
Wilaya ya Babati Mkoani Manyara, wakati wa hafla ya ufunguzi wa chuo
hicho iliyofanyika jana, mkoani Manyara.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano:- wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, akipanda mti wa kumbukumbu katika eneo la Chuo kipya cha VETA,
baada ya kufungua rasmi chuo hicho kilichojengwa Wilaya ya Babati mkoa
wa Manyara. Hafla ya ufunguzi wa Chuo hicho ilifanyika , mkoani Manyara.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akimsikiliza maelezo kutoka kwa Mwalimu wa ufundi wa Magari wa Chuo
kipya cha VETA cha Mkoani Manyara, Treekta dogo linalotumika kulimia na
kupandia Mbegu za mazao, wakati aliokuwa akitembelea na kukagua majengo
mapya ya Karakana ya chuo hicho baada ya kukifungua rasmi.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiwa katika picha ya pamoja kwa kumbukumbu na viongozi wa Chuo cha
Veta na viongozi wa Serikali baada ya ufunguzi rasmi wa chuo hicho
uliofanyika, mkoani Manyara. Picha na Sufian Muhidin
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)