Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Mohammed Gharib Bilal, akisoma
hotuba yake wakati akifungua Mkutano Mkuu
wa 28 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) ulioanza leo katika Hoteli ya Kunduchi Beach, jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wadau waliofika katika mkutano huo ambao umedhaminiwa na makampuni mbalimbali ikiwamo Benki ya NMB.
Waendesha shughuli hiyo, MC's, Ephraem Kibonde na Mavunde, wakiwa jukwaani wakati ratiba hiyo ikiendelea.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muunganowa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akimkabidhi kitabu cha muongozo wa maazimio ya kazi za Tawala za mitaa, Naibu Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI)
Agrey Mwanri, mara baada ya kufungua rasmi mkutano Mkuu wa 28 wa Jumuiya ya
Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) alioanza leo katika Hoteli ya Kunduchi Beach,
jijini Dar es Salaam. Katikati ni Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania,
Klaus-Peter BRANDES, (kulia) ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto,
Sophia Simba.
Wadau
na wafanyakazi wa Kampuni ya GF Trucks & Equipment Ltd Mohammed
Yusuph (kushoto) na mwenzake (kulia), wakiw ukumbini hapo wakati wa
ufunguzi huo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisalimiana na Meneja Mwandamizi wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya NMB,
Iman Kajula, wakati wakati alipokuwa
akitembelea na kuzindua mabanda ya maonyesho baada ya kufungua rasmi Mkutano wa
28 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) ulianza leo, katika
Hoteli ya Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam.
Makamu
wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Akisikiliza
maelezo kuhusu mashine za kufyatulia matofali ya gharama nafuu, kutoka kwa Mkurugenzi
wa Kampuni ya Rubana Construction, Ibrahim Sherally, wakati alipokuwa
akitembelea na kuzindua mabanda ya maonyesho baada ya kufungua rasmi Mkutano wa
28 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) ulianza leo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akizungumza na Mshauri wa TFDA, Octavian Soli, wakati alipokuwa akitembelea na
kuzindua mabanda ya maonyesho baada ya kufungua rasmi Mkutano wa 28 wa Jumuiya
ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) ulianza leo.
Picha ya pamoja baada ya ufunguzi.
Mdau
Ally akipozi na Mshkaji wake wakati wakiwa katika harakati za
maandalizi na utekelezaji wa majukumu na mahitaji ya wageni waalikwa
mahala hapo.
Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiondoka eneo la Viwanja vya Hoteli ya Kunduchi Beach, baada ya kufungua rasmi
Mkutano huo.Picha Na Muhidin Sufian
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)