Usafri wa treni utakuwa wa uhakika zaidi kuliko ilivyo sasa. Kwamba
wengi tutachagua kusafiri kwa treni kwa vile ni nafuu zaidi na salama
zaidi. Na ni usafiri rafiki kwa mazingira.
Siku hiyo inakuja kwa vile tunachoshindwa sasa ni kuwepo kwa wachache ' wanaohujumu' kwa makusudi usafiri wetu wa njia ya reli.
Mapato
yanayopatikana yanapotea. Kuna abiria wanaosafiri bila nauli zao
kuingia kwenye Shirika bali kwenye mifuko ya wanaojiita wajanja. Kuna
mizigo pia inayosafirishwa bila mapato yake kuingia kwenye Shirika,
bali, kwenye mifuko ya wanaojiita wajanja. Hali hiyo ni kwa reli ya kati
na reli ya Uhuru pia, kwa maana ya Tazara.
Na hao wanaojiita wajanja wengine ni viongozi tuliowapa dhamana za kusimamia mashirika yetu ya umma.
Siku hiyo inakuja tutakapokuwa na mfumo utakaohakikisha mwisho wa wanaojiita wajanja.
Hivyo
basi, siku hiyo inakuja tutakapoona fahari kusafiri kwa njia ya reli
yanayooendeshwa na mashirika yetu ya umma chini ya uongozi wa wazalendo
wa nchi hii watakaokuwa tayari hata kutoa fedha za mifukoni mwao
kuhakikisha treni zinatembea kwenye reli zetu.
Naam, siku hiyo inakuja....
Na hili ni Neno La Leo.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)