Hatimaye
safari ya kutafuta vipaji iliyo chini ya mpango wa tunzo za muziki za
Kilimanjaro, umefikia tamati mkoani mtwara juzi, ambapo washindi watatu
wa mkoa huo wamepatikana na kufunga kabisa mchakato huo kwa mwaka
huu. Huu ulikuwa ni mkoa wa tano kufanya mchakato huo, huku lengo likiwa
ni kuinua vipaji kutoka mikoani ambavyo mara nyingi imekuwa vigumu
kuvigundua kutokana na ufinyu wa mtandao wa habari au wakati mwingine
pia uwezo wa kiuchumi miongoni mwa wasanii hao.
Sasa katika
kuhakikisha kwamba muziki wa kitanzania unapelekwa kwenye kilele cha
mafanikio, kampuni ya bia Tanzania TBL kupitia kinywaji chake cha
Kilimanjaro Premium Lager mwaka huu ikaanzisha mchakato huo ambao
ulianza tarehe 22 Mei, ambapo kulikuwa na wataratibu wa kuchukua wasanii
watatu kila mkoa na kuwapandisha kwenye jukwaa la washindi wa tunzo wa
mwaka huu ambapo kila mkoa msanii mmoja alikuwa akichukuliwa kwa ajili
ya kushiriki tamasha kubwa ambalo linatarajiwa kufanyika jijini Dar es
Salaam wiki ijayo.
Majaji wa mchakato mzima.
Wakizungumzia
kwa nyakati tofauti kuhusiana na mchakato huo majaji Henry Mdimu,
Joseph Haule na Juma Kassim Kiroboto wamekiri kwamba Mtwara kumebarikiwa
kuwa na vipaji vya hali ya juu ukilinganisha na mikoa yote ambayo
mchakato umepita, ukilinganisha pia na idadi ya watu waliojitokeza,
Mtwara ilikuwa na idadi ndogo lakini wamefanya vema kuliko mikoa yote.
"Idadi kamili ya
washiriki waliojitokjeza Mtwara ni 55 tu lakini wote walikuwa wanaweza
na mwisho wa siku walikuwa wakifungana kwa alama za ushindi hali
iliyosababisha majaji kuwa na hali ngumu wakati wa kuchagua wasanii
watatu wa kuwakilisha mkoa kwenye tamasha la washindi", alikiri Henry
Mdimu ambaye alikuwa akiliongoza jopo la Majaji kwa kipindi chote cha
usaili.
Kuna kipindi majaji
walitamani kuongezewa idadi ya wasanii lakini kulingana na taratibu
walizopewa na waandaaji il;iwabidi kuumiza vichwa na mwisho wa siku,
Hassan Mohamed, Gift Julius na Nicolaus samwel ndio wakaibuka washindi
kwa mkoa wa Mtwara.
Kufuatia ushindi huo
watatu hawa watapoata nafasi ya kurekodi wimbo mmoja kila mmoja wao na
kisha kufanya wimbo wa kushirikiana ambao watauimba wakiwa kwenye
tamasha la washindi litakalofanyika mwishoni mwa wiki hii.
kwa mujibu wa
waandaaji, hili pia litakuwa ni tamasha la mwisho kwa mikoani ambapo
sasa, wiki ijayo kutakuwa na tamasha kubwa la washindi litakalofanyika
jijini Dar ambapo washindi hawa wa mikoani wataonesha uwezo wao wakiwa
jukwaa moja na washindi wa tunzo za muziki za Kilimanjaro za mwaka huu.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)