Mwenyekiti wa Alice Foundation akipokea chakula kutoka kwa Mch. Mkenda na wazee wa baraza la kanisa la Redeemed
Kanisa la Redeemded Gospel Church
tawi la Tanzania limeikabdihi Tassisi ya Alice Foundation msaada wa
vyakula kwa ajili ya kuwasaidia watoto wenye mahitaji mbalimbali na wale
wasiojiweza wanaoishi katika mazingira magumu na hatarishi.
Akikabidhi msaada huo leo
Mchungaji wa kanisa hilo lililopo Ubungo NHC mchungaji Damasus Mkenda
alisema kuwa kanisa kupitia wachungaji wake mbalimbali limeona kuwa kuna
hitaji kubwa lakuisaiida jamii ya watu wenye shida mbalimbali katika
kata ya Ubungo ambao wanahitaji chakula.
Alisema kuwa kanisa limeamua
kupitia Alice Foundation kutoa msaada huo kwa kuwa taasisi hiyo imekuwa
ikisaidia masuala mbalimbali ya kijamii katika kata ya Ubungo.
Msaada uliokabidhiwa ni pamoja na
mchele, Unga, Sukari, Maharage, Unga wa sembe, majani ya Chai ambapo
alisisitiza ili kuwa na jamii iliyobora inatakiwa watu wenye uwezo
kuwasaidia wale wasiokuwa nao.
"Sisi hili kanisa letu lina kila
sababu ya kuwasaidia watu wanaotuzunguka katika vitu mbalimbali kama
vile vyakula na mengineo muhimu, hivyo kwa sasa tumeanza na hili la
vyakula lakini kadiri muda unavyoenda tutawasaidia tena kwa vitu
mbalimbali ikiwa ni sehemu yetu ya mchango kwa jamii"alisema Mchungaji
Mkenda
Naye Mwenyekiti wa Alice
Foundation, Alice James Dosi alisema kuwa taaisi hiyo imekuwa
ikijishugulisha na masuala mbalimbali katika jamii ikiwa pamoja na
kuwasaidia watoto waishio katika mazingira magumu na hatarishi
,kuwezesha akina mama na masuala ya mazingira na masuala yanayohusu
MKUKUTA
Alisema kuwa katika kata ya Ubungo
kuna idadi kubwa ya watoto na watu wazima wenye mahitaji maalum ambapo
aliwataka watu wengine wajitokeze kusaidia masuala mbalimbali ya
kuwaendeleza watu hao..
Alisema kuwa kwa wale wenye
kuihitaji kutoa msaada kwa watoto hao na watu wenye mahitaji maalum kuwa
wanaweza kupiga simu namba 0713 022 558 au 0756 344 924 au wapige 0686 179111 au wafike katika ofisi za Alice Foundation zilizopo Ubungo (NHC)
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)