Katibu wa Bunge. Dkt. Thomas Kashililah, (wa pili kushoto) akimuongoza Katibu Mkuu Kiongozi
Balozi Ombeni Sefue, wakati akiingia mjengoni Bungeni kwa Waheshimiwa Wabunge. Balozi
Sefue jana alifanya ziara ya kutembelea jengo hilo la Bunge.
Katibu wa Bunge. Dkt. Thomas Kashililah akimuonesha katibu Mkuu Kiongozi
Balozi Ombeni Sefue sehemu za kukaa maofisa wa Serikali ndani ya Ukumbi wa Bunge kipindi wawapo ndani ya ukumbi huo
kusikiliza hoja mbalimbali zinazohusu Wizara zao.
Katibu wa Bunge. Dkt. Thomas Kashililah akimuonesha katibu Mkuu Kiongozi
Balozi Ombeni Sefue mtambo wa kudhibiti vipaza sauti pamoja na picha za video
Bungeni.
Mtaalamu wa mitambo ya Sauti na Picha kutoka Ofisi ya Bunge, Lemo
Toluwe, akimpa maelezo Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue ya namna mitambo
hiyo inavyofanya kazi Bungeni.
Mhandisi wa umeme kutoka Wakala wa Majengo wa Seriikali, Hijja
Mrutu, akitoa maelezo juu ya namna mitambo ya kufua Umeme Bungeni inavyofanya
kazi.
. Patson Sobha 'MCHUNGAJI' kutoka Idara ya Hansard, Bungeni akitoa maelezo kwa
Balozi Sefue ya namna Hansard inavyoandaliwa baada ya kunasa sauti za
majadiliano Bungeni.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akifurahia mitambo ya kisasa ya
kunasa picha za matukio yote katika viwanja vya Bunge.
Naibu waziri wa Miundombinu Mhe. Harrison Mwakyembe, akimsikiliza Katibu
Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue walipo kutana Bungeni juzi.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)