Waziri
wa Uchukuzi Omari Nundu (aliesimama) akifungua Mkutano wa kwanza wa
Baraza la Wafanyakazi la Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) April
12,2012 jijini Tanga, wenye wajumbe 70. Katika hotuba yake Waziri
amesema kwa kutamua umuhimu wa mfanyakazi katika kuongeza tija na
Ufanisi wa Mamlaka,wizara inampango endelevu wa mafunzo ,wenye lengo la
kukuza Ustadi na Uwezo wa Wafanyakazi katika kumudu mazingira yake ya
kikazi, Ili kufikia lengo hili Mamlaka yake hutenga fungu la fedha za
mafunzo, zisizoponua asilimia tano ya Bajeti yake ya kwaida ya kila
mwaka, hivyo katika mwaka 2012/13 Mamlaka inategemea kutumia sh.1.5
bilioni,
Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini Fadhili Manongi
akimkaribisha Waziri w a Wizara ya Uchukuzi Omari Nundu (hayupo
pichani ) kufungua mkutano wa kwanza wa Baraza la Wafanyakazi la
Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini Aprili 12,2012 ,jijini Tanga
Waziri
wa Uchukuzi Omari Nundu (kushoto) akiongea na Kaimu Mkurugenzi wa
Huduma za Usafiri kutoka Wizara ya Uchukuzi Saad Fungafunga (mwenye
Kaunda) wakati wa kufunguzi wa mkutano wa kwanza wa Baraza la
wafanyakazi la Mamlaka ya Usafiri wa Anga jijini Tanga –Apirili
12,2012.
Baadhi
ya wajumbe waliohudhuria ufunguzi wa mkutano wa kwanza wa Baraza la
Wafanyakazi la Mamlaka ya Usafiri wa Anga ambao unafanyika jijini Tanga
April 12,2012 na umefunguliwa na Waziri wa Uchukuzi Omari Nundu
(hayupo pichani) wajumbe 70 wanahudhuria.Picha na Mwanakombo
Juma-MAELEZO
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)