Na Mwandishi wetu
KAMPUNI ya Bia ya
Serengeti (SBL) imewataka watanzania kushiriki kwa nguvu zote katika
promosheni ya Vumbua Hazina ya Chini ya kizibo ili kuweza kushinda
zawadi mbali mbali.
Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Masoko wa Kambpuni ya SBL, Ephrahim Mafuru na
kusema kuwa SBL imetenga sh. Milioni 783 ambazo zitatolewa kama zawadi
kwa washindi wa promosheni hiyo ambayo itafanyika kwa wiki 16 kuanzia
Aprili 22.
Mafuru
alisema kuwa zawadi kwa wale watakao jishindia zawadi ya bia zina
thamani y ash. Milioni 265 zawadi za fedha taslim ni sh. Milioni 383.
Alisema kuwa pia watatoa pikipiki 16, Bajaj inane (8) , Jenereta nane
(8) na magari matatu aina ya Ford Figo.
Alisema kuwa ili
kuweza kuingia katika shindano hilo unatakiwa kununua bia zao,
Serengeti, Tusker au Pilsner na kukuta neno lenye tarakimu saba na
kulituma kwenda namba maalum ya 15317 na kuingia katika shindano hilo.
Mkurugenzi
Mtendaji wa kampuni ya Push Mobile, Freddie Manento aliipongeza SBL kwa
kuiteua kampuni yake kuendesha shindano hilo hasa kwa kuzingatia ubora
wa huduma zake.
Manento alisema kuwa kampuni yao ni bora zaidi katika kuendesha zoezi kama hilo na kuahidi kutoa hudima bora kwa wateja wake.
“Ni
faraja kubwa kufanya kazi na SBL katika shindano hili kubwa la
kuwazawadia wateja wa bidhaa zinazozalishwa na kampuni hiyo ya bia,
tutafikisha lengo lililowekwa,” alisema Manento.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)