Mmoja wa majeruhi wa kati ya 40
walionusurika kifo baada ya basi waliokuwa wakisafiri aina ya Coaster,
lenye nambari za usajili T 374 AVR, kupinduka lilipogongwa kwa nyuma na
basi jingine la kampuni ya El Saedy lenye nambari T 499 AVG. Tukio
lililotokea Aprili 23 mwaka huu saa moja asubuhi eneo la Imezu na Inyala
Wilaya ya Mbeya Vijijini.
Baadhi
ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Imezu wakikwa katika Hospitali ya
Rufaa, wakisubiri kupatiwa matibabu, mara baada ya basi aina ya Coaster
waliyokuwa wakisafirikia enye nambari
za usajili T 374 AVR, kupinduka lilipogongwa kwa nyuma na basi jingine
la kampuni ya El Saedy lenye nambari T 499 AVG. Tukio lililotokea Aprili 23 mwaka huu saa moja asubuhi eneo la Imezu na Inyala Wilaya ya Mbeya Vijijini.
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Imezu wakikwa katika
Hospitali ya Rufaa, wakisubiri kupatiwa matibabu, mara baada ya basi
aina ya Coaster waliyokuwa wakisafirikia enye
nambari za usajili T 374 AVR, kupinduka lilipogongwa kwa nyuma na basi
jingine la kampuni ya El Saedy lenye nambari T 499 AVG. Tukio lililotokea Aprili 23 mwaka huu saa moja asubuhi eneo la Imezu na Inyala Wilaya ya Mbeya Vijijini.
Basi aina ya Coaster waliokuwa wakisafiria abiria zaidi ya 40,
lenye nambari za usajili T 374 AVR, likiwa limepinduka baada ya
kugongwa kwa nyuma na basi jingine la kampuni ya El Saedy lenye nambari T
499 AVG. Tukio lililotokea Aprili 23 mwaka huu saa moja asubuhi eneo la
Imezu na Inyala Wilaya ya Mbeya Vijijini.
Basi aina ya Coaster waliokuwa wakisafiria abiria zaidi ya 40,
lenye nambari za usajili T 374 AVR, likiwa limepinduka baada ya
kugongwa kwa nyuma na basi jingine la kampuni ya El Saedy lenye nambari T
499 AVG.
Basi la kampuni ya El Saedy lenye nambari T 499 AVG lililohusika katika
ajali, baada ya kuligonga kwa nyuma basi aina ya Coaster enye nambari za usajili T 374 AVR ambapo zaidi ya abiria 40 kunusurika kifo.
Tukio lililotokea Aprili 23 mwaka huu saa moja asubuhi eneo la Imezu
na Inyala Wilaya ya Mbeya Vijijini.(Picha na Ezekiel Kamanga, Mbeya.)
*******
Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Abiria
zaidi ya 40 wamenusurika kifo baada ya basi waliokuwa wakisafiri aina
ya Coaster, lenye nambari za usajili T 374 AVR, kupinduka lilipogongwa
kwa nyuma na basi jingine la kampuni ya El Saedy lenye nambari T 499
AVG.
Kwa
mujibu wa mashuhuda wa basi la El Saedy likiwa katika hali ya
mwendokasi liliharibika mfumo wa breki kutoka eneo la Mlima Nyoka na
kuligonga basi hilo dogo kwa nyuma katika mteremko wa Shule ya Sekondari
Imezu, hali iliyopelekea basi hilo dogo kupinduka.
Baada
ya Coaster kupinduka basi la El Saedy likiwa bado katika mwendokasi
liliendelea na safari, kabla ya dereva kufanikiwa kulichepusha kabla
halijavuka reli ya TAZARA katika Kijiji cha Inyala Wilaya ya Mbeya
Vijijini.
Aidha
baadhi ya abiria katika basi hilo dogo walikuwemo wanafunzi 28, wa kike
na kiume wakielekea shuleni majira ya saa moja asubuhi, Aprili 23 mwaka
huu katika Shule ya Sekondari Imezu.
Mara
baada ya ajali hiyo kutokea baadhi ya abiria walikuwemo katika basi
hilo dogo walikimbizwa katika Hospitali ya Rufaa Jijini Mbeya, ambapo
kati yao wamelazwa ili kufanyiwa uchunguzi na wengine wakiruhusiwa
kurudi nyumbani.
Kaimu
Kamanda wa Jeshi la Polisi wa Mkoa wa Mbeya Barakiel
Masaki,hakupatikana kuelezea ajali hiyo ingawa dereva wa basi la El
Saedy anashikiliwa na Polisi kwa mahojiano.
Wakati
huo huo watroto watano waliokuwa wakioga katika mfereji wa Mwanjejele,
uliopo Igurusi Wilaya ya Mbarali, Aprili 22 mwaka huu majira ya saa tisa
alasiriwaliokota begi lililokuwa linaelea katika maji ya mfereji huo na
kukuta maiti ya mtoto mchanga.
Maiti
hiyo ikiwa imeharibika vibaya kutokana na kuoza ndipo walipolichukua
begi hilo na kulikabidhi katika Kituo cha Polisi cha Igurusi.
Hata
hivyo hakuna mtu yeyote aliyekamatwa kuhusika na tukio hilo, licha ya
wimbi la kuuawa kwa watoto wachanga Mkoani Mbeya limekuwa tatizo hali
inayosababisha vifo kwa watoto wasio na hatia.Na Ezekiel Kamanga wa Mbeya Yetu Blogu
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)