Bweni la wanafunzi lateketea kwa moto Handeni - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Bweni la wanafunzi lateketea kwa moto Handeni


WANAFUNZI takriban 50 wa Shule ya Sekondari Kidereko wilayani Handeni hawana sehemu ya kujihifadhi baada ya bweni lao kuteketea kwa moto pamoja na baadhi ya vifaa vyao vya shule.

Bweni hilo liliteketea kwa moto hivi karibuni majira ya asubuhi baada ya kutokea kwa hitilafu ya umeme kwenye bweni hilo muda ambao wanafunzi wote walikuwa wakiendelea na masomo darasani.

Akizungumza na Thehabari.com eneo la tukio Mwalimu wa Taaluma wa shule hiyo, Khamis Said amesema vitu vyote vya wanafunzi takribani 50 waliokuwa wakiishi katika bweni hilo viliteketea kwa moto, yakiwemo madaftari ya wanafunzi, nguo, magodoro na vitanda vya mbao viliteketea kwa moto.

“Hatukufanikiwa kuokoa kitu maana baada ya kusikika mlipuko na baadhi ya watu kuona moshi ukitoka ndani ya bweni hilo ambalo muda huo lilikuwa limefungwa tulikuta moto umesha tanda ndani na ukiwaka kwa kasi jambo hali ambayo ilikuwa ngumu kuokoa,” alisema Said.

Amesema kwa sasa wanafunzi hao wanasaidiwa na wanafunzi wenzao kimalazi huku wakiishi kwa shida kutokana na msongamano uliopo baada ya bweni lao kuteketea kwa moto. “Unajua baada ya ajali walibaki na nguo za shule walizokuwa wamevaa siku hiyo pamoja na madaftari ya vipindi vya siku hiyo tu, vifaa vingine vyote viliteketea kwenye ajali hiyo…shule imetoa baadhi ya fedha na kuwanunulia maitaji kadhaa japokuwa hayatoshelezi” alisema Mwalimu Said.

Hata hivyo alisema tayari uongozi wa idara ya elimu wilaya ya Handeni umetembelea eneo la tukio na wanafanya utaratibu wa kuwasaidia wanafunzi hao. Hii ni mara ya pili kutokea kwa majanga ya moto shuleni hapo kwani mwaka 2000 wanafunzi walichoma ofisi ya Mkuu wa Shule hiyo baada ya kuzuka kwa vurugu kati yao na uongozi wa shule.

Habari hii imeandaliwa na mtandao wa habari: www.thehabari.com

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages