Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi Ramadhani Khijjah akizungumza na viongozi mbalimbali
wa dini kuelezea umuhimu na ushiriki wao katika kufanikisha sensa ya
watu na makazi itakayofanyika kitaifa mwezi Agosti mwaka huu wakati wa mkutano wa viongozi wa dini unaoendelea jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi
mkuu ofisi ya taifa ya takwimu Dkt. Albina Chuwa akisisitiza jambo
kuhusu sensa ya watu na makazi itakayofanyika mwaka huu wakati wa semina
ya viongozi wa dini jijini Dar es salaam.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi Ramadhani Khijjah (kushoto)
akizungumza jambo na mkurugenzi mkuu wa ofisi ya taifa ya takwimu Dkt.
Albina Chuwa wakati wa mkutano wa mkutano wa viongozi wa dini
unaoendelea jijini Dar es salaam. Ofisi ya taifa ya takwimu imekutana na
viongozi hao kufuatia umuhimu na ushawishi wao katika jamii ili waweze
kushiriki kikamilifu katika kufanikisha sensa ya makazi itakayofanyika
mwezi Agosti 2012.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi Ramadhani Khijjah (kushoto) akiandika
maswali yaliyoulizwa na viongozi wa dini kuhusu namna serikali
ilivyojipanga kukamilisha sensa ya watu na makazi itakayofanyika
mwezi Agosti 2012. Wengine ni mkurugenzi mkuu wa ofisi ya taifa ya
takwimu Dkt. Albina Chuwa (katikati) na kamishna wa sensa Bi. Hajjat
Amina Mrisho
Baadhi ya viongozi wa dini wanaoendelea na mkutano wao jijini Dar es salaam wakipitia vitabu na vipeperushi vyenye jumbe mbalimbali kuhusu zoezi la sensa ya watu na makazi litakalofanyika nchi nzima mwezi Agosti mwaka huu baada ya wataalam kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu kutoa semina fupi kuhusu ushiriki wa viongozi hao katika kufanikisha sensa hiyo .
Viongozi
wa madhehebu mbalimbali ya dini nchini wakifuatilia kwa makini hotuba
ya Katibu mkuu wa Wizara ya Fedha na uchumi Ramadhani Khijjah alipokuwa
akizungumzia umuhimu wa sensa ya watu na makazi 2012 na namna serikali ilivyojipanga kukamilisha zoezi hilo kwa ufanisi.Picha na Aron Msigwa- MAELEZO
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)