Mchungaji
wa usharika wa kijitonyama Ernest Kadiva akifafanua jambo kwa
wanakamati ya maandalizi ya uzinduzi wa jengo la kitegauchumi cha
usharika huo litakalojulikana kama KIJITONYAMA LUTHERAN CENTRE(KLC)
litazinduliwa jumapili tarehe 29 mwezi huu,Ujenzi wa jengo hilo ulianza
mwaka 2009 na kugharimu jumla ya shilingi Bilioni 3.5.
Mchungaji
wa Usharika wa Kijitonyama Ernest Kadiva kushoto akibadilishana mawazo
na wajumbe wa kamati ya maandalizi ya uzinduzi wa jengo la Kijitonyama
Lutheran Centre(KLC)katikati Katibu wa baraza la kanisa hilo
Dkt.Victoria Kayombe na Mzee wa baraza la kanisa Leonard Shayo,wakati
walipokutana na waandishi wa habari kwa ajili ya kuwafahamisha juu ya
uzinduzi wa jengo hilo utakaofanyika Jumapili ya tarehe 29 mwezi huu.
Mjumbe
wa kamati ya utendaji ya Dayosisi ya Usharika wa Kijitonyama Dkt.Hans
Macha kulia akisisitiza jambo kwa Katibu wa Kamati ya maandalizi ya
uzinduzi wa jengo la Kijitonyama Lutheran Centre(KLC)Bw.Leonard Shayo
ambalo litatumika kama kitega uchumi wa kanisa hilo,Baada ya kumaliza
mkutano na waandishi wa habari kwa ajili ya kuwafahamisha juu ya uzinduzi wa jengo hilo utakaofanyika Jumapili ya tarehe 29 mwezi huu.
Katibu
wa baraza la kanisa hilo Dkt.Victoria Kayombe akiongea na baadhi ya
wanakamati ya maandalizi ya uzinduzi wa jengo la Kijitonyama Lutheran
Centre(KLC)litakalotumika kama kitega uchumi wa kanisa hilo,mara baada
ya kumaliza mkutano na waandishi wa habari juu ya uzinduzi wa jengo hilo
utakaofanyika Jumapili ya tarehe 29 mwezi huu,wa pili kutoka kushoto
Mchunga wa Usharika wa Kijitonyama Ernest Kadiva,Mwenyekiti wa kamati ya
maandalizi ya uzinduzi Selina Mkony,Mzee wa baraza la kanisa Leonard
Shayo na Mjumbe wa kamati hiyo Peniel Uliwa.Ujenzi huo umegharimu kiasi
cha Bilioni 3.5
Katibu
wa baraza la kanisa hilo Dkt.Victoria Kayombe akiongea na waandishi wa
habari kuhusiana na maandalizi ya uzinduzi wa Jengo la Kijitonya
Lutheran Centre(KLC)litakalotumika kama kitegauchumi wa Kanisa
hilo,Jengo hilo litazinduliwa rasmi Aprili 29,katikati Mchungaji wa
Usharika wa Kijitonyama Ernest Kadiva na Mwenyekiti wa ujenzi Bw.Sanyiel
Kishimbo.
Baadhi ya waumini na wanakamati wa maandalizi ya uzinduzi wa jengo la
Kijitonyama Lutheran Centre(KLC)walioudhuria kwenye mkutano na waandishi
wa habari juu ya maandalizi ya uzinduzi wa Jengo hilo litakalozinduliwa
Jumapili ya tarehe 29 mwezi huu.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)