Afisa
mauzo wa Airtel kanda ya kati bw Hillary Tarimo akimkabithi vitabu vya
taaluma bw Leonard Cyprian Ngotta Mwalimu wa taaluma shule ya sekondari
Hurui katika halfa fupi iliyofanyika katika shule ya Sekondari Gubali
ambapo Airtel kupitia programme ya shule yetu imegawa vitabu kwa shule
za sekondari nne ziliziko wilaya ya kondoa mkoa wa Dodoma, shule
zilizopatiwa vitabu ni pamoja na Goma, Gubali,Itaswi na Hurui,
akishuhudia katika ni Kessy Musilenga Kessy Makamu mkuu wa shule ya
Sekendari Gubali
Afisa
mauzo wa Airtel kanda ya kati bw Hillary Tarimo akimkabithi vitabu vya
taaluma bwana Ibrahim Juma Mwesi Mwalimu mkuu wa shule ya sekondari
Itaswi katika halfa fupi iliyofanyika katika shule ya Sekondari Gubali ambapo
Airtel kupitia programme ya shule yetu imegawa vitabu kwa shule za
sekondari nne ziliziko wilaya ya kondoa mkoa wa Dodoma, shule
zilizopatiwa vitabu ni pamoja na Goma,Hurui, Gubali na Itaswi,
akishuhudia katika ni Kessy Musilenga Kessy Makamu mkuu wa shule ya
Sekendari Gubali
Airtel
yatoa msaada wa vitabu shule za secondari wilaya ya Kondoa- Dodoma
Chini ya mpango wake wa shule yetu kampuni ya simu za mkononi ya Airtel
imetoa vitabu vya ziada na kiada kwa shule 4 za sekondari zilizoko
wilaya ya kondoa mkoani Dodoma ili kusaidia maendeleo ya elimu wilayani
hapo na katika kutoa huduma kwa jamii.
Makabithiano
hayo yalifanyika katika halfa fupi iliyofanyika katika shule ya
Sekondari Gubali na shule ya sekondari zilizonufaika na msaada huo ni
pamoja na sekondari ya Goma, Gubali,Itaswi na Hurui, zote za wilayani
humo ambapo wawakilishi wa shule hizo walikabidhiwa vitabu vyenye
thamani ya shilling milioni moja kwa kila shule.
Akiongea
katika hafla ya makabithiano Afisa uhusiano wa Airtel T Afisa mauzo
kanda ya kati bw Hillary Tarimo alisema" Airtel kwa kupitia programme
ya shule yetu imeweza kuwafikia wanafunzi wengi na shule nyingi nchini
Tanzania na leo tunafurahi kuwa sehemu ya maendeleo ya shule za
sekondari wilayani Kondoa na kuweza kuchangia vitabu zitakavyotumika
katika kufundishia na kuwa nyenzo muhimu kwa walimu na wanafunzi wa
shule zitakazokabithiwa.
Tutaendelea
kushirikiana na Serikali chini ya Wizara ya Elimu katika kuinuia na
kuboresha kiwango cha elimu nchini kwani tunatambua elimu ndio ufunguo
wa maisha na vijana ndio nguvukazi ya kesho. Aliongeza Tarimo.
Naye
Makamu mkuu wa shule ya sekondari Galibu Bw Kessy Musilenga alisema"
nachukua fulsa hii kuwashukuru Airtel kwa kutufikia na kutoa msaada wa
vitabu kwa shule zetu na kupunguza changamoto zilizokuwepo katika shule
hizi, tunayofuraha kwa shule yetu na wenzetu wa shule za jirani
zilizopo wilayani kondoa kupata nyenzo muhimu ambazo zitainua kiwango
cha elimu kwa wakazi na wanafunzi wa wilayani"
Tunawaasa
wanafunzi kuvitumia vizuri vitabu hivyo ili vilete matokeo vizuri kwa
wanafunzi, Tunaamini jamii ikipata elimu bora maendeleo ya shughuli
mbalimbali za uchumi yatafanyika kwa ufanisi zaidi na kuleta mafanikio
makubwa kwa jamii. Aliongeza Kessy.
Kampuni
ya simu za mkononi ya Airtel imekuwa ikitoa misaada mbalimbali kama
vile Vitabu vya shule ya sekondari, siku chache zilizopita Airtel
ilitoa msaada wa computer 20 na vitabu vyenye thamani ya million 10 kwa
chuo kikuu cha Dodoma - UDOM hii ni katika kurudisha faida inayoipata
na kuchangia katika huduma kwa jamii.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)