---
VIONGOZI
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), wamesema wameamua
kukataa rufaa dhidi ya hukumu ya Hukumu ya Mahakama Kuu ya Tanzania
Kanda ya Arusha iliyotolewa wiki hii ambayo ilimuondoa madarakani Mbunge
wa chama hicho Arusha Mjini Godbless Lema.
Rufaa hiyo wanataraji kuikata hivi karibuni katika Mahakama kuu ya Rufaa Tanzania.
Wakihutubia
umati mkubwa wa wakazi wa Arusha na viunga vyake waliofruka katika
viwanja vya NMC, mapema leo viongozi hao akiwepo Godbless Lema mwenye
aliwasihi wananchi kuendelea kuwa watulivu na kuondoa hofu na anaimani
watashinda.
Mahakama
Kuu Kanda ya Arusha ilitoa hukumu hiyo na kutengeua Ubunge wa
Godbless Lema baada ya kumkuta na hatia ya kutumia lugha ya
udhalilishaji na maneno ya kashifa dhidi ya mgombea wa Balozi Dk.
Batilda Buriani katika uchaguzi wa mwaka 2010 alipokuwa akigombea kwa
tiketi ya CCM.
Mwenyekiti
wa Taifa wa Chama hicho Freeman Mbowe alisema zipo sababu tatu
zilizowafanya waende kukata Rufani badala ya kuingia kwenye uchaguzi
mdogo moja kwa moja.
Mbowe
alisema kwamba hawawezi kuacha tu bila kukata rufaa na kukimbilia
katika uchaguzi mdogo maana kufanya hivyo ni kukubaliana na maamuzi ya
kihuni yaliyotolewa ili kuchezea fedha za Watanzania.
“Tukiingia
kwenye uchaguzi mdogo ndugu zangu tutakuwa tunakubali kuwa Lema
alishinda kwasababu alidhalilisha wanawake katika jimbo la Arusha,
kitendo ambacho sisi hatuamini,” alisema Mbowe .
Akitaja
sababu ya pili alisema upo ukweli kuwa Serikali ya CCM imejaa ufisadi
hivyo imekuwa haioni gharama za kutumia mabilioni ya fedha kwa ajili ya
chaguzi ndogo.
Alisema
kama wao wakiamua kuingia katika uchaguzi mdogo ni wazi kuwa watakuwa
wameruhusu matumizi makubwa ya fedha za wananchi masikini yatumike
wakati nafasi ya kukata Rufani walikuwanayo.
“CCM
wanakimbilia kujilipa posho wawapo kwenye uchaguzi mdogo, sasa kwa
vile ukitaka Rufani unasubiria majibu mawili, Rufani inaweza
kuturudishia mbunge wetu au ikaitupa Rufani yetu hayo ni mamuzi
yanayoweza kupatikana huko,” alisema Mbowe.
Mara
baada ya kuwasili Lema aliyeingia na uwanjani hapo akiwa na gari yake
Mercedez Benz namba za usajili T776 BNK na upande wa pili akiwa na
Mbowe pekee, alizungumza na halaiki hiyo Lema alisema yeye yupo tayari
kupigania haki katika maisha yake kwa wakati wote awapo hai.
Alisema
ana amini kuwa wananchi wa Arusha na maeneo mengine wameumia kwa
kitendo dhalimu kilichofanywa na Jaji mmoja kukubali kupindisha ukweli
kwa faida ya kundi la watu wachache.
“Sintaingia
kwenye ofisi zao, njooni nyumbani na mahali popote tutakapokutana
tutafanya kazi ya wananchi waliotuchagua kwa kura nyingi.Nimevuliwa
ubunge kihuni na kwa hira sasa Mungu atachukua uhao wao,” alisema Lema.
Lema
alisisitiza kuwa yeye bado ni mbunge, licha ya kuvuliwa ubunge huo na
Jaji lakini ataendelea kufanya kazi. “niwaambie mimi bado ni mbunge
wenu na nitaendelea kufanya kazi kama kawaida”.
Aidha
Mbunge huyo aliyevuliwa wadhifa wake na mahakama alisema huku
akishangiliwa na umati mkubwa wa watu Lema aliwaambia wananchi hao
kwamba katika kipindi atakachokuwa akisubiria uamuzi wa Rufani yake
Mahakama ya Rufani Tanzania, atahakikisha moto aliouwasha unasambaa nchi
nzima.
“Nitahakikisha
anakula mihogo, kutembea kwa miguu ili nifike nchi nzima, sasa kwa
vile wao wamechokoza basi mimi nitahakikisha ninafia porini kama noma
acha iwe noma na ndio imeanza ya kuhakikisha nchi inabadilika.
“Sasa
Arusha harakati ndio zimeanza kama walifikiria tulikuwa tunataka
ubunge imekula kwao, wamenitia hasira na sasa hii nchi inaenda kugeuka.
Kwa
upande akizungumzia uamuzi wa kutaka Rufani alisema, huo ni uamuzi
sahihi kwani kama asipokata rufani atakuwa ametenda dhambi ya kubariki
hukumu bandia kuendelea kubakia kwenye kumbukumbu za Mahakama.
“Kilichoniondoa
ubunge ni sheria kuchakachuliwa sasa nisipo kata Rufani nitakuwa
nimetenda dhambi kubwa ya kubariki uchakachuaji huo,” alisema Lema.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)