Mbunge wa Jimbo la Ubungo na Mkurugenzi wa Habari na Uenezi(CHADEMA) Mh John Mnyika
---
Chama
Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinatoa taarifa kwa umma kwamba
uchukuaji na urejeshaji wa fomu za kugombea ujumbe wa Bunge la Afrika
Mashariki (EALA) kupitia CHADEMA umekamilika tarehe 6 Aprili 2012 saa 10
Jioni.
Uteuzi wa mwisho wa wagombea utafanyika tarehe 9 Aprili 2012 siku ya
jumatatu kuanzia saa 3 asubuhi ambapo wagombea wote waliorudisha fomu
wametaarifiwa kufika kwenye mkutano husika.
Wagombea
waliorudisha fomu mpaka sasa ni pamoja na Godfrey Mnubi, Edgar William
Chibura, John Simon Malanilo, Patrick Lubango Nkandi, Anna E.
Maghwira, Deogratias George Assey, Pasquina Ferdinand Lucas, Deusdedit
Jovin Kahangwa, Antony Calist Komu na Mwantum Khamis Mgonja.
Ikumbukwe kuwa tarehe 12 Machi 2012 Katibu wa Bunge alitoa Taarifa kwa
Umma kwamba,Uchaguzi wa wajumbe tisa (9) watakaoiwakilisha Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki utafanywa na
Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, wakati wa Mkutano wake wa Saba
utakaofanyika Dodoma, kuanzia tarehe 10 hadi 20 Aprili, 2012.
Uchaguzi
huo wa Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki unafanyika kwa kuzingatia
kuwa maisha ya Bunge hilo lililoingia madarakani mwaka 2006 yatafikia
ukomo wake 04 Juni, 2012.
Taarifa imetolewa kwa vyombo vya habari na: John Mnyika(MB)
Mkurugenzi wa Habari na Uenezi
07/04/2012
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)