TAARIFA KUTOKA IKULU - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

TAARIFA KUTOKA IKULU

Rais Jakaya Mrisho Kikwete amewasili  mjini Blantyre ,Malawi  leo jioni kuhudhuria  Mazishi ya Profesa Bingu  wa Mutharika, aliyekuwa Rais wa Malawi., aliyefariki tarehe 5 April, 2012  Kufuatia matatizo ya Moyo

Rais Kikwete ni miongoni mwa Viongozi wakuu Saba kutoka nchi jirani na Malawi.

Nchi hizo ni Afrika Kusini, Benin, Kenya, Msumbiji, Zimbabwe na Zambia.

Wakati huohuo Ikulu inapenda kukanusha taarifa zilizonukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari kudai kuwa Rais ametofautiana na Waziri Mkuu kuhusu aina ya hatua za kuwachukulia Mawaziri wanaotuhumiwa na ubadhirifu katika Wizara zao.

Napenda kueleza Umma kuwa taarifa hizo si za kweli.
Pia  nitumie nafasi  hii kuwatahadharisha waandishi wa habari  kuwa makini, waangalifu na wachambuzi wakati wa kupokea, kusikiliza na kuandika au kutangaza taarifa wanazopata.

Rais kikwete aliwasili kutoka Brazil alipokuwa amekwenda Kwa Ziara ya kikazi ya siku tano tarehe 21 April, 2012.

Kwa hivyo basi Rais hajapata taarifa yeyote rasmi kutoka kwa Waziri Mkuu, na bado anasubiri kupewa taarifa hyo rasmi Kwa vile suala la tuhuma hizo limetokea Bungeni.

Na kama kuna Waziri ambaye ameandika barua ya kujiuzulu, basi atakua amemuandikia Rais na kama zipo Rais ndiye atakaye zipokea na kuamua hatua inayofuatia.

Kwa hivyo sio busara hata kidogo kwa vyombo vya habari kueneza uongo na fitna zenye lengo la kuchonganisha si viongozi tu , bali  hata viongozi na wananchi kwa ujumla.

Rais Kikwete anatarajia kurejea nchini kesho  tarehe 23 April mara baada ya maziko.
.............................
Mwisho


Imetolewa na Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi
Blantyre -Malawi.
22 April, 2012

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages