TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Gazeti
la Tanzania Daima la leo Jumapili Aprili 22, 2012 lina habari katika
ukurasa wake wa mbele yenye kichwa cha habari ‘JK alinda Mawaziri’,
inayodai kumekuwa na mazungumzo baina ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete na
Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda kuhusu hatua inayopaswa kuchukuliwa dhidi
ya mawaziri waliotakiwa kujiuzulu.
Habari
hiyo imedai kuwa Mhe. Pinda anataka mawaziri wanaokabiliwa na tuhuma
waondoke ili kuleta uwajibikaji serikalini, lakini, imeendelea kudai
habari hiyo, â€Å“Rais Kikwete amesema mawaziri hao waachwe waendelee na
kazi zao, kwa kuwa suala hili ni la upepo tu, liachwe litapitaâ€.
Tunachukua
nafasi hii kuweka bayana kwamba habari katika hilo hazeti la Tanzania
Daima Jumapili si za kweli, bali ni za uzushi na upotoshaji mkubwa.
Mheshimiwa
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, ambaye alikuwa katika ziara ya kikazi
nchini Brazil, amerejea jana Aprili 21, 2012 jioni. Hajaonana wala
kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu, Mhe. Pinda.
Hivi sasa Mhe. Rais anasubiri kupata taarifa rasmi kutoka Bungeni Dodoma.
Mhe Rais anawasihi wananchi wasiamini habari hizo za upotoshaji zilizomo kwenye gazeti hilo la Tanzania Daima Jumapili.
Pia
ametoa rai kwa wanahabari wasitoke nje ya mstari wa weledi katika
kutekeleza kazi zao ili kuendelea kulinda heshima zao binafsi, vyombo
wanavyofanyia kazi pamoja na taaluma yenyewe.
Imetolewa na
Mkurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu
.Dar es Salaam
.
22 Aprili, 2012
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)