Baadhi
ya washiriki wa Semina ya kuwahamasisha Watanzania kubuni miradi
inayokopeshwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB wakijiandikisha
kushiriki semina hiyo iliyoandaliwa na Taasisi ya Sekta Binafsi nchini
TPSF Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti
wa Bodi wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini TPSF, SALUM SHAMTE
(Katikati) akiwa na washiriki wengine wa Semina iliyoandaliwa na TPSF
ili kuhamasisha Watanzania kubuni miradi inayokopeshwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB iliyofanyika Jijini Dar es Salaam
Waziri
wa Fedha na Uchumi MUSTAFA MKULO akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi wa
Taasisi ya Sekta Binafsi nchini TPSF, SALUM SHAMTE wakati wa Semina
iliyoandaliwa na TPSF ili kuhamasisha Watanzania kubuni miradi inayokopeshwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB iliyofanyika Jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi
Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB, TONIA KANDIERO akizungumza
na washiriki wa Semina iliyoandaliwa na Taasisi ya Sekta Binafsi nchini
TPSF ili kuhamasisha Watanzania kubuni miradi inayokopeshwa na benki hiyo.
Waziri
wa Fedha na Uchumi MUSTAFA MKULO akisisitiza jambo kwa baadhi ya
washiriki wa semina iliyoandaliwa na Taasisi ya Sekta Binafsi nchini
TPSF ya kuhamasisha Watanzania kubuni miradi inayokopeshwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB iliyofanyika Jijini Dar es Salaam .
Na Mwandishi Wetu
Serikali
imesema imeweka mpango kabambe unaohusisha sekta ya umma na sekta
binafsi kuweza kushirikiana ili kuweka vivutio vingi vitakavyowezesha
nchi kukuza uchumi wake na wa mtu mmoja mmoja kupitia fursa mbalimbali
za kiuwekezaji zilizopo.
Akizungumza
kwenye semina iliyoandaliwa na Taasisi ya Sekta Binafsi nchini TPSF kwa
kushirikiana na Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB yenye lengo la
kuwahamasisha Watanzania kubuni miradi inayokopeshwa na benki hiyo,
Waziri wa Fedha na Uchumi MUSTAFA MKULO amesema sheria inatoa fursa kwa
wadau kuitumia benki hiyo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini BI
ESTHER MKWIZU amesema awali Watanzania walikuwa hawajui kama kuna
utaratibu wa miradi ya watu binafsi kuweza kukopeshwa na Benki ya
Maendeleo ya Afrika.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)