Mkuu
wa mkoa wa Singida Dkt. Parseko Kone akizungumza kwenye hafla ya
uzinduzi wa kituo kipya cha macho kilichopo katika hospitali ya mkoa
mjini Singida. Kulia ni katibu tawala mkoa Liana Haasa na kushoto ni
mganga mkuu wa mkoa Dkt. Doroth Kujugu.
Mganga
wa macho mkoa wa Singida Dkt. Dismas Kimvule akitoa taarifa yake
kwenye hafla ya uzinduzi wa kituo kipya cha macho mjini Singida.
Mwakilishi
wa shirika la International Centre for Eye Care Education (ICEE)
Afrika Mashariki Dkt. Naomi Nsubuga akizungumza kwenye hafla ya
uzinduzi wa kituo kipya cha macho.
Mkuu
wa mkoa wa Singida Dkt. Parseko Kone akizindua rasmi kituo cha macho
kilichopo kwenye hospital ya mkoa mjini Singida. Kulia ni Mwakilishi wa
ICEE Naomi Nsubuga na wa kwanza kushoto ni Dkt. Nkunde Mwakyusa kutoka
wizara ya afya na ustawi wa jamii.
Baadhi ya viongozi waliohudhuria uzinduzi wa kituo kipya cha macho kilichopo katika hospitali ya mkoa.
Kikundi
cha uhamsishaji cha afya club kikitoa burudani kwenye hafla ya
uzinduzi wa kituo kipya cha macho mjini Singida.Picha na Habari na
Nathaniel Limu
-------
Mkuu
wa mkoa wa Singida Dkt. Parseko Kone ameuagiza uongozi wa hospitali ya
rufaa ya mkoa wa Singida kuhakikisha watoto wa umri chini ya miaka
mitano wenye matatizo ya macho, wanapelekwa haraka kwenye hospitali
zenye huduma kwa watoto hao.Dkt. Kone ametoa agizo hilo wakati
akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa kituo cha upimaji wa macho
(Vision centre), kilichopo katika hospitali ya rufaa ya mkoa mjini
Singida.
Amesema
kwa vile huduma hiyo haipatikani katika hospitali ya rufaa ya mkoa kwa
watoto wenye umri huo ni muhimu watoto hao wakaharakishwa kupelekwa
kwenye hospitali zenye uwezo wa kuwahudumia.
Dkt.
Kone ametaja hospitali hizo kuwa ni pamoja na KCMC ya Moshi, hospitali
ya taifa ya Muhimbili na CCBRT zote za jijini Dar es salaam.
Aidha,
Dk. Kone ametumia fursa hiyo kuwashukuru wafadhili ambao wamekuwa
wakitoa msaada wa nauli ya kwenda na kurudi kwenye hospitali hizo kwa
watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano walio na matatizo ya macho.
“Ukizungumzia
matatizo ya macho katika mkoa wetu wa Singida, huwezi kuacha kutaja
jina la Mbunge wa Singida Mjini Mh. Mohammed Dewji kutokana na mchango
wake mkubwa ambao ameendelea kuutoa kwa watu wanaokabiliwa na matatizo
ya macho. Nachukua nafasi hii kumpongeza na namwomba aendeleze misaada
hiyo kwa wakazi wa mkoa huu” amesema Dkt. Kone.
Awali
mratibu wa taifa wa huduma za macho kutoka wizara ya afya na ustawi wa
jamii Dkt. Nkunde Mwakyusa, amesema kuwa wizara kwa kushirkiana na
wadau wa huduma za macho nchini, imeandaa mpango mkakati wa taifa wa
miaka mitano wa huduma za macho nchini, ambao umeanza kutekelezwa Julai
mwaka jana.
Amesema
lengo la mpango mkakati huo, ni kuboresha utoaji wa huduma za macho
hapa nchini kwa kuzingatia utatuzi wa changamoto zilizopo. Uboreshaji
huo utafuata sera ya afya inayelekeza ushirikishwaji wa sekta binafsi
katika huduma ya afya.Kwa mujibu wa Dkt. Mwakyusa, Shirika lisilo la
kiserikali la International Center for Eye Care Education (ICEE)
limetoa msaada wa vifaa katika kituo hicho cha kutolea huduma ya macho
ili kuboresha huduma.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)