Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akiwa katika picha ya pamoja na Mawaziri aliowaapisha waliosimama,hafla hiyo ilifanyika jana Ikulu Mjini Zanzibar,wengine Makamo wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif,(kushoto) na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi,(kulia).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akimuapisha Mhe,Ramadhan Abdalla Shaaban,kuwa Waziri wa Ardhi.Makaazi,Maji na Nishati,katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar jana,kabla Shaaban,alikuwa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akimuapisha Mhe,Ali Juma Shamuhuna,kuwa Waziri wa Elimu na Mfunzo ya Amali,katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar jana,kabla Shamuhuna,alikuwa Waziri wa Ardhi,Makazi Maji na Nishati.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akimuapisha Mhe,Suleiman Othman Nyanga,kuwa Waziri wa Kilimo na Maliasili,katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar jana,kabla Nyanga,alikuwa Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi na Waziri asiyekuwa na Wizara Maalum.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akimuapisha Mhe,Abdilah Jihad Hassan,kuwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi,jana Ikulu Mjini Zanzibar,kabla Jihad alikuwa Waziri wa Habari,Utalii, Utamaduni na Michezo.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu]
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)