Mkurugenzi
wa Uendelezaji Biashara wa Shirika la Nyumba la Taifa, Bwana David
Shambwe (katikati) akitoa maelezo ya Mradi wa Nyumba za makazi zilizopo
Ilala Mchikichi jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Meneja wa Masoko
na Utafiti wa NHC, Bwana Itandula Gambalagi na kulia ni Meneja wa Mauzo
wa NHC, Bwana William Genya.
Kwa
mara nyingine Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) leo (Jumanne, 24 April
2012) linazindua rasmi mauzo ya nyumba katika mradi wake mpya wa
Mchikichi, Ilala jijini Dar es Salaam. Ujenzi wa mradi huo unatarajiwa
kukamilika rasmi Februari, 2013.
Mradi
huu upo eneo la Mchikichini karibu na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam, huduma zote muhimu za kijamii jijini Dar es Salaam zikiwamo za
kiafya, shule, maduka, uwanja wa ndege na masoko. Pia Mradi huu
unatarajiwa kuboresha maisha ya wanunuzi wa nyumba hizi kwani upo
karibu kabisa na katikati ya jiji, nyumba zipo ndani ya uzio kwa ajili
ya usalama wao na kuna maegesho ya magari ya kutosha .
Mradi
una nyumba 48 tu zitakazouzwa, kila nyumba ina vyumba vitatu vya
kulala. Kila nyumba ina ukubwa wa mita za mraba 115.8 (sq.m), sebule
kubwa yenye veranda, chumba kimoja cha kulala kinachojitegemea, vyumba
viwili vya kulala, (vinavyotumia choo cha pamoja), jiko kubwa la kisasa
na eneo la kufulia na kuanikia nguo.
Sifa
za ziada za mradi huu ni kuwa na eneo la watoto kuchezea, eneo maalum
la kukusanyia taka, maegesho ya magari ya ziada. Kila nyumba itauzwa
kwa bei ya Sh 168,239,748.62 (bila VAT).
Tunawahamasisha
wenye kuhitaji nyumba hizi wafanye mawasiliano na makao makuu ya
shirika na kukamilisha taratibu mapema kwaajili ya kuweza kuingia
kwenye mchakato ulio wazi wa manunuzi. Uzinduzi wa mauzo ya nyumba za
mradi huu ni mfululizo wa uzinduzi wa miradi ya NHC unalenga kutimiza
malengo ya mkakati wa Shirika wa miaka mitano ya kujenga nyumba 15,000
ambazo kati ya hizo, nyumba 10,000 ni za wananchi wa kipato cha kati na
cha juu na 5,000 kwa ajili ya wananchi wa kipato cha chini.
Ukiwa
mdau na mnunuzi mtarajiwa, ama una ndugu/rafiki anayetamani kununua
nyumba katika mradi huu, tafadhali wasiliana na kitengo cha mauzo makao
makuu simu namba 0754 444 333; barua pepe: sales@nhctz.com na pia tembelea tovuti ya shirika www.nhctz.com kwa maelezo zaidi.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)