Meneja
kampeni wa kampuni ya Push Mobile, Talib Rashid (katikati) akifafanua
jambo kuhusiana na Bahati Nasbu ya Simba kwa kutumia ujumbe mfupi wa
meseji ambapo mshindi atazawadiwa pikipiki aina ya Bajaj. Zawadi
nyingine katika bahati nasibu hiyo ni pikipiki na fedha taslim Sh.
50,000 zitakazotolewa kila siku kwa muda wa siku 90. Kulia ni Katibu
Mkuu wa Simba Evodius Mtawala na kushoto ni Swed Mkwabi ambaye ni mjumbe
wa kamati ya utendai ya klabu hiyo. Picha na Mpiga picha wetu
***************************************
Na Mwandishi wetu
KAMPUNI
ya Push Mobile kwa kushirikiana na klabu ya Simba imezindua kampeni ya
bahati nasibu kwa mashabiki wa timu hiyo ambapo mshindi atajinyakulia
pikipiki aina ya bajaji yenye thamani ya Tsh 6 Milioni.
Akizindua
kampeni hiyo leo kwenye ofisi za Push Mobile Kinondoni jijini Dar es
Salaam, Katibu Mkuu wa Simba, Evodius Mtawala alisema kampeni hiyo
itasaidia kuwaweka pamoja na wanachama wa klabu hiyo kongwe hapa nchini.
Mtawala
alisema falsafa ya simba ambayo ni timu ya wananchi ni kuwa karibu na
wanachama wake popote duniani hivyo kampeni hiyo itasaidia kuiweka
karibu zaidi klabu hiyo na wanachama wake .
Naye
Meneja wa Kampeni hiyo kutoka Push Mobile, Talib Rashid alisema droo
kubwa ya bahati nasibu hiyo itachezeshwa baada ya siku 90 na mashabiki
wa simba wanatakiwa kuandika ujumbe mfupi wa maneno (SMS) yenye neno
Simba na kuituma kwenda namba 15678 ili kuingia katika droo hiyo.
Rashid
alisema mbali na zawadi hiyo pia mashabiki hao watajinyakulia zawadi ya
pesa taslimu tsh 50,000 kila siku ndani ya siku 90 pia washindi wengine
wawili watajinyakulia pikipiki zenye thamani ya tsh 1.5 Milioni kila
moja.
"Kampeni
hii itahusisha mashabiki wa klabu ya simba ambao watatakiwa kujibu
maswali ambayo baada ya kutuma neno Simba kwenda namba 15678 watatumia
kwenye simu zao," alisema Rashid.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)