Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akimtazama mtoto anayepata matibabu ya kansa
katika Hospitali ya watoto wanaougua ugonjwa huo iliyopo mjini Brasilia
nchini Brazili. Hospitali hiyo ambayo inapokea wagonjwa 4000 kwa mwezi
inatibu asilimia sabini ya kansa na hivyo kuwawezesha wagonjwa ambao ni
watoto kuendelea kuishi.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa amembeba mtoto Anna Julia Telles
mwenye umri wa miezi mitatu anayepata matibabu ya kansa katika Hospitali
ya watoto wanaougua ugonjwa huo iliyopo mjini Brasilia nchini Brazili.
Hospitali hiyo inatoa dawa aina ya chemotherapy kwa wagonjwa ambao ni
watoto 500 kwa mwezi na inatibu asilimia sabini ya kansa.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi wa
Hospitali ya watoto wanaougua ugonjwa wa kansa Marli Aparecide dos
Santos mara baada ya kumaliza ziara yake ya kutembelea hospitali hiyo
iliyopo mjini Brasilia nchini Brazili. Hospitali hiyo inatibu asilimia
sabini ya kansa na hivyo kuwawezesha wagonjwa ambao ni watoto kuendelea
kuishi.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akiangalia moja ya bidhaa zinazouzwa na
Hospitali ya watoto wanaougua ugonjwa wa kansa kwa ajili ya kupata fedha
za kuwasaidia watoto hao huku Afisa ubalozi wa Tanzania nchini Brazili
Tabu Makata akimuangalia. Hospitali hiyo iliyopo mjini Brasilia nchini
Brazili inatoa dawa aina ya chemotherapy kwa wagonjwa ambao ni watoto
500 kwa mwezi na inatibu asilimia sabini ya kansa.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akimsikiliza mfanyakazi wa Hospitali ya
watoto waougua ugonjwa wa kansa akielezea jinsi hospitali hiyo pamoja na
jamii inavyotoa huduma ya kujitolea kwa wagonjwa. Hospitali hiyo
iliyopo mjini Brasilia nchini Brazili inatoa dawa aina ya chemotherapy
kwa wagonjwa ambao ni watoto 500 kwa mwezi na inatibu asilimia sabini ya
kansa.Picha na Anna Nkinda - Maelezo.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)