Ndugu zangu,
Na
ikafika siku ya mikate isiyotiwa chachu. Siku hiyo Mwana- Kondoo wa
Pasaka huchinjwa. Yesu akawatuma Petro na Yohana, akawaagiza, `` E
nendeni mkatuandalie chakula cha Pasaka.'' Wakamwuliza, ``Tukaandae
wapi?''
Yesu
akawajibu, ``Mtakapokuwa mnaingia mjini, mtakutana na mwanaume
aliyebeba mtungi wa maji. Mfuateni huyo huyo mpaka kwenye nyumba
atakayoingia. Kisha mwambieni mwenye nyumba; Mwalimu anauliza, kiko
wapi chumba cha wageni, ambamo mimi na wanafunzi wangu tutakula Pasaka?
Atawaonyesha chumba kikubwa ghorofani. Chumba kilicho na fanicha zote.
Fanyeni maandalizi humo.''
Basi, wakaenda, wakakuta kila kitu kama Yesu alivyokuwa amewaambia. Hivyo, wakaandaa chakula cha Pasaka.Wakati ulipofika, Yesu akaketi mezani pamoja na wanafunzi wake kumi na wawili. Kisha akawaambia;
Basi, wakaenda, wakakuta kila kitu kama Yesu alivyokuwa amewaambia. Hivyo, wakaandaa chakula cha Pasaka.Wakati ulipofika, Yesu akaketi mezani pamoja na wanafunzi wake kumi na wawili. Kisha akawaambia;
``Nimetamani
mno kuila Pasaka hii pamoja nanyi kabla ya kuteswa kwangu. Kwa maana,
nawaambieni, hii ni mara yangu ya mwisho kula Pasaka mpaka maana halisi
ya Pasaka itakapokamilika katika Ufalme wa Mungu.''
Hapo
Yesu akapokea kikombe cha divai, akashukuru akisema, ``Chukueni mnywe
wote. Kwa maana, nawaambieni, tangu sasa sitakunywa tena divai hadi
Ufalme wa Mungu utakapokuja.'' Alitamka Yesu.
Na hilo ni Neno La Leo. Nawatakia nyote Pasaka Njema!
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)