Katibu
wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa
habari jijini Dar leo,Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, mtaa wa
Lumumba, Dar es Salaam, kuhusu maamuzi ya kikao cha Kamati Kuu ya CCM
iliyokutana leo mjini Dar es Salaam, ambapo pamoja na mambo mengine
imeridhia Rais Kikwete kuvunja Baraza la Mawqaziri.
Rais
amepokea taarifa na maazimio ya Kamati ya wabunge wa CCM na Kamati ya
uongozi ya wabunge wa CCM juu ya kilichotokea kwenye bunge lililopita
mjini Dodoma.
Taarifa
hizo zimewasilishwa kwenye kamati kuu na kujadiliwa. Pamoja na taarifa
hizo kamati Kuu imepokea taarifa ya jinsi Rais alivyojipanga kuchukua
hatua za kuwawajibisha mawaziri na watendaji wa serikali na wale wa
mashirika ya umma waliobainika kuhusika na ubadhirifu ulioinishwa na
taarifa ya Mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za Serikali, Kamati za
kudumu za bunge na wabunge bungeni.
Kamati Kuu imeamua yafuatayo;
1.
Kamati Kuu inatambua na kuheshimu haki na wajibu wa wabunge kujadili
utendaji wa serikali yao.Inapongeza juhudi za serikali kuhakikisha kuwa
ripoti ya mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali inajadiliwa kwa
uwazi na hivyo kuibua mapungufu yaliyojadiliwa.
2.
Kamati Kuu imeridhika na imebariki uamuzi wa Rais KULISUKA UPYA BARAZA
LA MAWAZIRI na taasisi zingine zilizoanishwa katika ripoti hizo.
Imesisitiza utekelezaji wa uamuzi huo ufanywe mapema iwezekanavyo.
Aidha
kamati Kuu imeipongeza Kamati Teule ya baraza la wawakilishi Zanzibar
iliyoundwa kuchunguza utendaji katika sekta mbalimbali kwenye serikali
ya mapinduzi Zanzibar kwa taarifa yao.
Kamati
Kuu inawapongeza wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kwa jinsi
walivyojadili taarifa hiyo na pia Kamati Kuu inaipongeza Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar kwa kuipokea taarifa na kuanza kuifanyia kazi.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)