Fukwe
za Ziwa Tanganyika kwa Mkoa wa Rukwa ni fursa pekee ambayo bado
haijaharibiwa au kutumiwa vya kutosha. Ukanda huu ni kielelezo tosha cha
mandhari na fursa nzuri za uwekezaji katika eneo hili ambalo kwa kiasi
kikubwa linachochewa na ujenzi wa barabara za lami zinazoendelea
kujengwa katika Mikoa hii itakayounganisha Mikoa hiyo na Ziwa Tanganyika
pamoja na Nchi jirani zilizopakana na Ziwa hilo.
Baadhi
ya Hoteli zinazopatikana Mkoani Rukwa katika Wilaya ya Nkasi katika
Tarafa ya Kipili. Boti zinazoonekana ni kwa ajili ya wateja
watakaohitaji kwenda kucruise ndani ya Ziwa. Bado yapo maeneo maalum
ambayo yametengwa kwa ajili ya ujenzi wa Hoteli za Kitalii katika ukanda
huu.
Hakika mandhari haya yanavutia na hivyo ni baadhi ya vyumba katika Hoteli hiyo ya Kipili.
Ukanda
wa Ziwa Tanganyika unajumuisha mikoa ya Rukwa, Katavi na Kigoma.
Mikoa hii kwa pamoja ni Mikoa iliyopitiwa na Ziwa Tanganyika ambalo
fukwe zake ni sehemu ya Utawala katika Mikoa hiyo. Ziwa hilo kwa upande
wa pili limepakana na Nchi jirani za Kongo, Zambia na Burundi pamoja na
Rwanda. Miongoni mwa fursa kuu zinazopatikana humo ni pamoja na uvuvi,
usafirishaji katika Mikoa na nchi hizo. Fukwe zake ambazo zimehifadhiwa
ni fursa pekee ya Ujenzi wa Hoteli za Kitalii kutokana na Watalii wengi
kupenda kutembelea maeneo hayo. Hali kadhalika kuna samaki wa mapambo.
Kubwa zaidi kunakadiriwa kuwepo kwa mafuta ya Petroli na Gesi,
Utafiti bado unaendelea kufanywa na Kampuni ya Beach Petroleum kwa
kushirikiana na TPDC Tanzania kubaini uwepo wa rasilimali hizo. Katika
Ziwa hili ndiko inakopatikana Meli Kongwe kuliko Meli zote Duniani, Meli
ya MV Liemba inakadiriwa kuwa na umri zaidi ya miaka 100 huku bado
ikiwa inafanya kazi.
Mbunge
wa Jimbo la Nkasi Kaskazini Ally Kessy, Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia
Stella Manyanya, Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Joyce Mgana na Kamati ya Ulinzi
na Usalama ya Wilaya ya Nkasi wakimaliza ziara ya kukagua Fukwe za Ziwa
Tanganyika huku wakielekea kwenye Hoteli ya Kipili ambayo kwa kiasi
kikubwa hupata wageni wa kitalii.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya Kushoto na Mkuu wa Wilaya ya
Nkasi Joyce Mgana wakiwa wamejipumzisha katika moja ya maeneo ya
mapumziko kwenye Hoteli ya Kipili baada ziara ya kuzungukia fukwe za
Ziwa Tanganyika.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya (Kulia) na Mkuu wa Wilaya
ya Nkasi Joyce Mgana (Kushoto) wakiongea na watalii waliofikia
katika Hoteli ya Kipili Wilayani Nkasi siku za hivi karibuni walipoenda
kutembelea fukwe hizo.Picha na Habari na Hamza Temba-Ofisi ya Mkuu wa
Mkoa Rukwa
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)