Mmoja
wa wagonjwa waliolazwa katika Hospitali ya Temeke, Zainabu Abbasi
pamoja na mwanawe, Kheri Hasifu wakipokea boksi la sabuni ya kufulia
kutoka kwa Meneja wa Benki ya NBC Kanda ya Ilala, Gaudence Shawa, wakati
wafanyakazi wa NBC walipofika hospitalini hapo kukabidhi msaada wa
vifaa vya tiba na sabuni na kushiriki shughuli za usafi jan. Kulia ni
Katibu wa Afya wa hospitali hiyo, Lucy Sozigwa.
Mmoja
wa wafanyakazi wa benki ya NBC, Ali Lwano, akigawa sabuni kwa baadhi
ya wagonjwa waliolazwa katika Hospitali ya Temeke, wakati wa hafla hiyo
fupi ambayo NBC ilikabidhi msaada wa vifaa vya tiba na sabuni na
kushiriki shughuli za usafi hospitalini hapo.
Wafanyakazi
wa benki ya NBC, Janeth Mutahanamilwa (katikati) na Emmanuel Mseti
(kulia kwake) wakigawa sabuni kwa baadhi ya wagonjwa na watoto wao
waliolazwa katika Hospitali ya Temeke.
Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya NBC wa Kanda ya Ilala wakisafisha mazingira ya hospitali hiyo wakati wa hafla hiyo.
Baadhi
ya wafanyakazi wa benki ya NBC wa Kanda ya Ilala na watumishi wa
Hospitali ya Temeke wakipozi kwa picha katika hafla ambayo NBC
ilikabidhi msaada wa vifaa vya tiba na sabuni na kushiriki shughuli za
usafi hospitalini hapo Dar es Salaam jana. Matawi yaliyoshiriki katika
hafla hiyo ni, hiyo Corporate, Mnazi Mmoja, Kichwele, Samora,
Industrial, Kariakoo, Muhimbili, Chang’ombe na Mbagala.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)