Ziara ya Waziri wa Muungano, Samia Saluhu Kisiwani Pemba - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Ziara ya Waziri wa Muungano, Samia Saluhu Kisiwani Pemba

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano Samia Suluhu Hasani (kulua), akipata maelezo kutoka kwa Afisa Mipango wa Wilaya ya Mkoani,  Bw.  Amour  kuhusu mradi wa usambazaji umeme huko Magomba katika Jimbo la Mkanyageni Mkoa wa Kusini Pemba.
Waziri  Samia Suluhu Hasani akizunguza jambo na Mbunge wa Jimbo la Mkanyageni, Habib Juma Mnyaa (kulia) mara baada ya kumaliza kungalia usambaji wa umeme katika vijiji vya jimbo hilo mradi ambao umefadhiliwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jimbo (CDCF).
Waziri Samia Suluhu Hasani  akionyeshwa Bwawa wakati wa ukaguzi wa Mradi wa Ufugaji wa Samaki unaofadhiliwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), huko Chambani Kisiwani Pemba.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano, Samia Suluhu  akipata maelezo juu ya kilimo cha kisasa cha migomba katika Tikundi cha Ushirika cha Tukubaliane cha Nfikiwa Jimbo la Wawi, Bw.  Ali Juma Nasor ambaye ni Mratibu wa Mradi wa ASSP/ASDL Wilaya ya Chake Chake.
Waziri Suluhu akivuka Mtaro wakati wa ukaguzi wa Ufugaji wa Samaki.
Mchuuzi katika Soko la mbogamboga liliopo Furaha Wawi, Bi. Amina Khamis  (kushoto), akitoa ufafanuzi wa jambo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mungano,m Samia Suluhu Hasani kuhusu hali ya biashara katika soko hilo. Picha zote na Ali Meja

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages