Mkurugenzi
wa Chuo Cha Biashara za Nje cha Nchini India (IIFT) Thomas Chako
akiongea katika mahafali ya 12 ya Shahada ya Uzamili inayotolewa na
chuo hicho kwa ushirikiano na Chuo Cha Usimamizi wa Fedha (IFM ) cha
Dar es salaam. Chako alikabidhi veti kwa wahitimu takribani 31. Wengine
pichani kutoka kulia ni Makamu wakuu wa Chuo cha IFM Prof. Jairo na
Prof. Tadeo Satta na Mkuu wa Chuo hicho Prof Godwin Mjema. Chako
alihimiza umuhimu wa Tanzania kuzalisha wataalamu wa kutosha wa biashara
za kimataifa ili kunufaika na fursa za biashara za ulimwengu.
Mathew
Shayo(Kulia)akipokea cheti chake cha kuhitimu shahada ya uzamili ya
usimamizi wa biashara za kimataifa kutoka Chuo Kikuu cha Biashara za
Kimataifa cha India (IIFT) kutoka kwa Mkurugenzi wa Chuo hicho. Thomas
Chako katika hafla iliyofanyika mwishoni mwa wiki Dar es Salaam. IIFT
huendesha kozi hiyo ya MBA-IB kwa ushirikiano na Chuo Cha Usimamizi wa
Fedha (IFM) cha Dar es salaam. Wanaoshuhudia ni Makamu wakuu wa Chuo cha
IFM, Profesa Isaya Jairo (wa pili kulia) na Profesa Tadeo Satta. Chako
alihimiza umuhimu wa Tanzania kuzalisha wataalamu wa kutosha wa
biashara za kimataifa ili kunufaika na fursa za biashara za ulimwengu.





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)