Katibu wa Bunge anatoa Taarifa kwa Umma kwamba, Uchaguzi
wa wajumbe tisa (9) watakaoiwakilisha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
katika Bunge la Afrika Mashariki utafanywa na Wabunge wa Bunge la
Jamhuri ya Muungano, wakati wa Mkutano wake wa Saba utakaofanyika
Dodoma, kuanzia tarehe 10 hadi 20 Aprili, 2012.
Uchaguzi
huo wa Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki unafanyika kwa kuzingatia
kuwa maisha ya Bunge hilo lililoingia madarakani mwaka 2006, yatafikia
ukomo wake 04 Juni, 2012.
Pamoja
na Taarifa hii, Katibu wa Bunge ambaye ndiye Msimamizi wa Uchaguzi
huo, atatoa Tangazo kwenye Gazeti la Serikali kwa mujibu wa masharti
yanayohusika, kuhusu siku ya uteuzi, ambayo ni tarehe 10 Aprili, 2012, saa kumi (10.00) Jioni, na pia kuhusu siku ya uchaguzi ambayo ni tarehe 17 Aprili, 2012 saa tano (5.00) Asubuhi, mara au mapema baada ya Kipindi cha Maswali.
Aidha,
katika Tangazo hilo, Katibu wa Bunge pia atatoa masharti yanayopaswa
kuzingatiwa na Wagombea wa Vyama vyote vya Siasa vyenye uwakilishi
Bungeni kuhusiana na Uchaguzi huo, kwa ajili ya kuviwezesha kuanza
mchakato wa kuwapata Wagombea kupitia Vyama hivyo, ambao majina yao
yatawasilishwa Bungeni kwa ajili ya kupigiwa kura.
Kwa
Taarifa hii, watu ambao wanazo sifa za kugombea na kuchaguliwa kuwa
Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki wanaweza kuanza mchakato wa
kuteuliwa kuwa wagombea wa uchaguzi huo, kupitia Vyama vyao vya Siasa.
Taarifa hii imetolewa na
Idara ya Habari, Elimu kwa Umma na Ushirikiano wa Kimataifa,
Ofisi ya Bunge





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)