Bi.
Harriet Macha kutoka Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC)
akifafanua lengo la ziara hiyo ambapo amesema ni muhimu kwa wanafunzi na
vizazi vijavyo kujua historia na madhara yaliyotokana biashara ya
utumwa. Katika kuadhimisha kumbukumbu ya biashara ya utumwa duniani
Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa kimegharamia ziara ya wanafunzi
kutoka shule tatu jijini Dar es Salaam kwenda kutembelea kituo cha
Kihistoria cha Kaole kilichopo Bagamoyo.
Mtaalamu wa Mambo ya Kale Bw. Jumanne Majige akitoa maelezo kwa wanafunzi.
Wanafunzi
wakishangaa kisima cha maajabu. Ksima hicho kiliaminika kuwa cha
maajabu baada Serikali kuwahi kuchota takribani Lita 10,000 za maji
lakini kiwango cha maji hayo hakikupungua.
Wanafunzi
wakinawa maji ya katika kisima cha maajbu kwa imani ya kuwa ni yenye
baraka. Kisima hichi hakikauki maji wala kuongezeka tangu enzi za
ukoloni na kinaaminika kuwa ni cha maajabu.
Bw.
Jumanne Majige akitoa maelezo kwa wanafunzi kuhusu Kaburi la wapendanao
waliokufa siku moja kwenye bahari ya Hindi na kuzikwa pamoja lililopo
Kaole Bagamoyo.
Mti wa Mbuyu unaosadikiwa kuwa na miaka 500.
Stella Vuzo kutoka Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa
akizungumza na waanafunzi kutoka shule za Benjamini Mkapa, Kibasila,
Lugalo na Mbezi . Katika mazungumzo hayo akizungumzia lengo la Umoja wa
Mataifa kuwa ni pamoja na kuhakishasha biashara ya Utumwa inatokomezwa
kabisa na kuwaasa vijana wajijengee utamaduni wa kusoma vitabu na
kuzijua haki zao za msingi na kujitambua.
Bi. Vuzo alitoa changamoto hizo katika ziara hiyo ambapo
pia alitoa fursa hiyo kuwasilisha ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa
Mataifa aliutoa katika maadhimisho ya siku ya kuwakumbuka wahanga wa
biashara ya utumwa duniani inayodhimishwa kila mwaka tarehe 25 mwezi
Machi.Picha na Habari Kwa HIsani ya Full Shangwe Blogu





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)