Taswira Zaidi Za Muendelezo Wa Kampeni Za CCM -Kata ya Kikatiti Arumeru Mashariki - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Taswira Zaidi Za Muendelezo Wa Kampeni Za CCM -Kata ya Kikatiti Arumeru Mashariki

 SISI NI CCM DAMU: wanafunzi wa kidato cha pili shule ya sekondari Kikatiti wakishadadia CCM wakati wa mkutano wa kampeni za CCM Kata ya Kikatiti
 Msanii wa TOT anayekwenda kwa jina la Juakali, akihamasisha watu, baada ya mgombea wa CCM Arumeru Mashariki, Sioi Sumari na Mratibu kampeni za CCM Mwigulu Nchemba (kulia) kupanda jukwaani katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo Kata ya Kikatiti A Town.
 Sioi akikasalimia katoto kwenye mkutano huo
 Mgombea ubunge wa CCM jimbo la Arumeru Mashariki, Sioi Sumari akiwasalimia wapigakura wake, kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kijiji cha Mikandini jimboni humo. Kulia ni Mratibu wa kampeni za CCM jimboni humo, Mwigulu Nchemba.
 NI CCM TU: Kina mama na kina baba wa kijiji cha Mikandini wakishangilia  kwenye mkutano uliofanyika katika kijiji hicho.
 Wazee wa Kijiji cha Maroroni jimbo la Arumeru Mashariki  wakifuatilia kwa makini hotuba ya mgombea wa CCM wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye kijiji hicho.
Wananchi wa Kijiji cha  Maroroni wakiwa wameketi kwenye mawe ili kuweza kupata kwa undani zaidi hotuba ya mgombea wa CCM Sioi Sumari kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika katika kijiji hicho.
Msafara wa mgombea wa CCM ulichanja mbuga katika maeneo ya Kata ya Kikatiti kusaka kura jimboni Arumeru Mashariki.Picha na Bashir Nkromo-Arumeru

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages