TASWIRA ZA UZINDUZI WA KAMPENI ZA CCM HUKO ARUMERU LEO - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

TASWIRA ZA UZINDUZI WA KAMPENI ZA CCM HUKO ARUMERU LEO

Mwenyekiti wa CCM na Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa akizindua kampeni za CCM za uchaguzi mdogo jimbo la Arumeru Mashariki leo katika Uwanja wa Ngaresero.
Wananchi wa Arumeru Mashariki wakiwa wamefurika kwenye mkutano wa uzinduzi wa kampeni za CCM leo.
Mwenyekiti Mstaafu wa CCM, Rais Mstaafu Benjamin Mkapa akimnadi mgombea ubunge wa tiketi ya CCM jimbo la Arumeru Mashariki, Sioi Sumari kwenye uzinduzi wa kampeni za CCM za uchaguzi huo kwenye Uwanja wa mpira wa Ngaresero leo.
Mmoja wa walioshiriki kura za maoni kupata mgombea wa CCM, Elirehema Kaaya (kulia) akimpongeza mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM Arumeru Mshariki Sioi. wakati wa uzinduzi wa kampeni hizo.
Pamela Sioi Sumari akimnadi mumewe Sioi Sumari wakati wa uzinduzi wa kampeni hizo za CCM. Pamela ni mtoto wa Waziri Mkuu wa Zamani Edward Lowassa.
Sioi akihutubia kwenye mkutano huo wa uzinduzi wa kampeni za CCM.
Masanja wa Orijino Komedi akifanya manjonjo yake mbele ya umati, wakati wa uzinduzi wa kampeni za CCM leo.(Picha zote na Bashir Nkoromo)

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages