Shughuli Za Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Huko Zanzibar - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Shughuli Za Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Huko Zanzibar

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Balozi Seif Ali Iddi akizungmza na Viongozi wa CCM WA Mkoa wa Kaskazini Pemba Kwenye Ukumbi wa Skuli ya Micheweni Pemba.Kushoto yake ni Mwenyekiti wa CC Mkoa wa Kaskazini Pemba Nd. Mberwa Hamad Mberwa, kulia yake ni Mjumbe wa Kamatiya Siasa ya Mkoa huo Mh. Dadi Faki Dadi na Pembeni yake ni Mke wa Balozi Seif Mama Asha Suleiman Iddi.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akikabidhi mchango wa Shilingi 1,000,000/- kwa Mwalimu wa Madrasatul Jabal Hira ya Utaani Wete Ustaadhi Khamis Hamad Faki kwa ajili ya kusadia uendelezaji wa Madrasa hiyo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Baadhi ya Viongozi wa Madrasatul Jabal Hira ya Utaani Wete Pemba ambapo alikuwa Mgeni rasmi katika Maulidi ya Chuo hicho kutukuza Uzawa wa Mtume Muhammad { SAW }.
Waumini mbali mbali wa Dini ya Kiislamu wakimsalia Mtume Muhammad { SAW } katika hafla ya Maulidi ya Uzawa wa Kiongozi huyo iliyoandaliwa na Madrasatul Jabal Hira iliyopo Mtaa WA Utaani Wete Pemba ambapo Mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar balozi Seif Ali Iddi.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akifurahia kazi za mikono zinazoendeshwa na Kikundi cha Ushirika cha Tuvumiliane Women Group kiliopo Mjini Wete akiwa pamoja na Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi. Balozi Seif alihamasika kuchangia shilingi 500,000/- wakati Mama Asha akachangia shilingi 300,000/- kuuendeleza Ushirika huo.
Katibu wa Ushirika wa Ufugaji Samaki wa Kishakaashishangi wa Kiuyu Minungwini Nd. Othman Bakari akimpatia maelezo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ai Iddi jinsi ya harakati za Mradi wao ulioanzishwa mwaka 1994.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kikagua Maendeleo ya Ujenzi wa Tuta la kuzuia Maji ya Bahari yasivamie mashamba ya Kilimo cha Mpunga katika Bonde la Mziwanda Wilaya ya Micheweni

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages