Na Mwandishi Wetu
SERIKALI
imeipongeza Kampuni ya Heineken Afrika Mashariki kwa kuiteua Tanzania
kuwa miongoni mwa nchi zinazotembelewa na Kombe la UEFA, huku ikiiomba
kuwekeza kwenye sekta ya michezo hapa nchini hususan, timu ya taifa ya
wanawake, Twiga Stars.
Pongezi
na maombi hayo yalitolewa juzi usiku na Naibu Waziri wa Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara, katika hafla ya
kulishuhudia kombe hilo iliyofanyika kwenye Hoteli ya Kilimanjaro Kempinski jijini Dar es Salaam.
Dk.
Mukangara alisema wanatambua uwepo wa Heineken hapa nchini, kwani
wanaziona bidhaa zao, hivyo kwa namna moja ama nyingine wanachangia
uchumi wa nchi kupitia kodi.
Alisema kwa uamuzi huo wa kulileta kombe hilo maarufu duniani, wameongeza chachu na hamasa ya michezo hapa nchini, lakini litakuwa jambo bora kama watawekeza kwenye michezo hapa nchini na kuisaidia Twiga Stars, hasa ukizingatia inajituma na kuonyesha kiwango bora.
Katika
hafla hiyo, ambayo waalikwa walipata nafasi ya kupiga picha na kombe
hilo, ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali, akiwemo Waziri wa Nchi Ofisi
ya Rais Utawala Bora, Mathias Chikawe, Mbunge wa Bariadi Magharibi, John
Cheyo, Mkurugenzi wa Michezo, Leonard Thadeo, Kaimu Katibu Mkuu wa TFF,
Sunday Kayuni, Mwenyekiti wa Yanga, Lloyd Nchunga, Mwenyekiti wa Soka
la Wanawake, Lina Madina Mhando na wengineo.

.jpg)




No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)