Teddy
Mapunda mkurugenzi wa Mawasiliano na uhusiano wa Kampuni ya bia ya
Serengeti (SBL) akizungumza na waansdishi wa habari hawapo pichani baada
ya uwekajiwa jiwe la msingi katika hospitali ya Wilaya ya Iringa mjini
kwa ajili ya ujenzi wa matanki katika mradi wa kuvuna maji ya mvua kwa
ajili ya hospitali hiyo na wakazi wa karibu na hospitali hiyo iliyopo
Frelimo kata ya Mwangata mjini Iringa.
Naibu
Waziri wa Maji Injinia Gryason Rwenge akiweka jiwe la msingi katika
hospitali ya Wilaya ya Iringa mjini kwa ajili ya ujenzi wa matanki
katika mradi wa kuvuna majiya mvua kwa ajili ya hospitali hiyo na
wakazi wa karibu na hospitali hiyo iliyopo Frelimo kata ya Mwangata
mjini Iringa, wanaoshuhudia kutoka kulia ni Nandi Mwiyombela Meneja
Miradi Endelevu na uwajibikaji wa kampuni ya bia ya Serengeti (SBL),Dk.
Stella Kiwele Mganga mkuu msaidizi wa hospitali hiyo na Teddy Mapunda
mkurugenzi wa Mawasiliano na uhusiano wa (SBL).
Hii
ndiyo Hospitali yenyewe na hawa ni baadhi ya wauguzi na wafanyakazi wa
hospitali hiyo mara baada ya kuhudhuria uwekaji wa jiwe la msingi.
Mradi huo kuwezesha zaidi ya watu 150,000 kupata maji safi na salama
Kampuni
ya Bia ya Serengeti (SBL) kupitia mradi wake wa EABL Foundation leo
imezindua mradi wa uvunaji maji katika hospitali ya Frelimo ya Manispaa
ya Iringa ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya maji duniani
itakayoadhimishwa tarehe 22 Machi 2012.
Zaidi
ya watu wapatao 150,0000 wanaohudumiwa na hospitali hiyo watanufaika.
Maadhimisho ya wiki ya maji nchini Tanzania yafanyika kitaifa mjini
Iringa.
Mradi
huu wa uvunaji wa maji ya mvua ulifikiwa baada ya kushauriana na
Wizara ya maji na Manispaa na kutambua wingi wa maji yanayopotea ambayo
yangeweza kuvunwa kwa matumizi.
Mradi
unatarajiwa kutumia kiasi cha zaidi yashilingi milioni 50 ikiwa ni
gharama za ununuaji na uwekaji wa matanki ya maji, mabomba, pampu ya
umeme na ukarabati mdogo wa miundo mbinu iliyopo. Kampuni
ya bia ya Serengeti inafahamu na inatambua umuhimu wa maji duniani na
hata katika biashara yetu, na ndio maana basi tunashiriki kikamilifu
katika kuhamasisha upatikanaji wa maji safi na salama.
Kwa
mwaka huu pekee Kampuni ya Bia ya Serengeti imetenga zaidi ya shilingi
milioni 300 katika miradi ya maji.Kati ya hizo, shilingi milioni 100
ni kwa ajili ya udhamini wa wiki ya maji ambazo zimetumika katika
matangazo , mabango ya matangazo , fulana, kofia , vipeperushi ,
vijarida n.k.
Kiasi
kilichobaki cha shilingi milioni 200 ni kwa ajili ya miradi endelevu
ya maji katika mikoa ya Iringa , Mwanza, Moshi na Dar es Salaam. Kama
kampuni inayowajibika ,tumekuwa tukijihusisha na miradi mbalimbali ya
maji safi na salama ukiwemo ule wa Mkuranga. Na pia tumeshiriki katika
mradi wa kuboresha maji katika Hospitali ya Amana kwa kushirikiana na
makampuni mengine na mashirika yasiyo ya kiserikali.
Katika
mradi wa Mkuranga , Kampuni ya Bia ya Serengeti imewekeza zaidi ya
shilingi milioni 384.6 ambapo zaidi ya watu 250,000 wananufaika na
mradi huu.
Kampuni
ya Bia ya Serengeti itaendelea kufadhili miradi endelevu ya kuisadia
jamii hasa miradi ya maji, ili kwa pamoja tuweze kupunguza na kuboresha
miundombinu na upatikanaji wa maji safi na salama.






No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)