RAIS JAKAYA KIKWETE KATIKA TUZO ZA (AJET) USIKU HUU DIAMOND JUBILEE - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

RAIS JAKAYA KIKWETE KATIKA TUZO ZA (AJET) USIKU HUU DIAMOND JUBILEE


 Rais Jakaya Kikwete akiongea na Fili Karashani Mwandishi mkongwe naambaye ameshinda  tuzo ya Maisha ya Mafanikio katika Tasnia ya Habari mwaka 2011, katika tuzo za (EJAT) zilizoandaliwa na Baraza la Habari Nchini Tanzania (MCT) na washirika wake, hafla hiyo inafanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee usiku huu, katika picha kushoto ni Mwandishi wa siku nyingi Khamis Ben Kiko.


 Rais Jakaya Kikwete akimkabidhi Nevil Meena cheti cha ushindi wa jumla kwa katika tuzo hizo mara baada ya kutangazwa rasmi.


 Kikundi cha Ngoma za asili cha Simba Thietre kikitumbuiza katika tuzo hizo.


 Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) Teddy Mapunda akikabidhi tuzo kwa mwandhishi wa habari wa Mlimani Radio Tuma Dandi mshindi wa habari za watu wenye ulemavu- Redio


 Mhariri wa gazeti la Tanzania Daima Absalom Kibanda akikabidhi tuzo kwa Abdallah Majura Mkurugenzi wa Radio Sports FM ya Dodoma.


Kaimu Mkurugenzi Mtendaji na Mkurugenzi wa Fedha wa Kampuni ya bia ya Serengeti Graham Anderws akimkabidhi cheti na zawadi yake Nevil Meena kutoka gazeti la Mwananchi.


 Mkurugenzi wa kampuni ya Executive Solution Agrey Maleale akimkabidhi zawadi yake Khamis Hamad kutoka magazeti ya Uhuru na Mzalendo.


 Katibu Mtendaji wa MCT Bw. Kajubi Mukajanga akizungumza katika hafla hiyo.


Rais Jakaya Kikwete akizungumza na Mkurugenzi wa Makampuni ya IPP Bw. Reginald Mengi walipkutana katika hafla hiyo.Picha Zote na Full Shangwe Blogu

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages