
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
leo, akiomuonesha maendeleo ya ujenzi wa barabara nchini katika ramani
ya Tanzania Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB),
Bi. Mary Consolata Muduuli (wa pili kulia) Ikulu, Dar es Salaam, leo
Machi 31, 2012. Bi. Muduuli ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa AfDB kwa
nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Seychelles, Rwanda, Ethiopia na
Eritrea, alifuatana na Mwakilishi wa Benki hiyo katika Tanzania. Bi.
Tonia Kandiero ( wa pili kushoto) na mshauri wa Mkurugenzi Mtendaji
huyo, Bi. Salma M Salum. Picha na IKULU
--
--

Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
leo, Jumamosi, Machi 31, 2012, amekutana na kufanya mazungumzo na
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Bi. Mary
Consolata Muduuli.
Katika
mazungumzo hayo yaliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam, Bi. Muduuli ambaye
ni Mkurugenzi Mtendaji wa AfDB kwa nchi za Tanzania, Kenya, Uganda,
Seychelles, Rwanda, Ethiopia na Eritrea, alifuatana na Mwakilishi wa
Benki hiyo katika Tanzania. Bi. Tonia Kandiero na mshauri wa Mkurugenzi
Mtendaji huyo, Bi. Salma M Salum.
Katika
mazungumzo hayo, Rais Kikwete ameishukuru AfDB kwa misaada mingi ya
maendeleo ambayo Benki hiyo imekuwa inatoka kwa Tanzania, na ameitaka
kuendelea kusaidia jitihada za Watanzania kujiletea maendeleo.
Benki
hiyo ambayo ilianza shughuli zake katika Tanzania mwaka 1971 hadi
mwishoni mwa mwaka jana ilikuwa imeidhinisha miradi 121 yenye thamani ya
dola za Marekani bilioni tatu katika sekta za miundombinu,
usafirishaji, kilimo, maji, huduma za kijamii, umememe, viwanda na
madini na mawasiliano.
Tokea
Machi mwaka huu, 2012, AfDB imeidhinisha miradi 16 ambayo 14 kati yao
imeanza kutekelezwa na miwili bado haijaanza kutekelezwa. Miongoni mwa
miradi miwili ambayo haijaanza kutelekezwa ni pamoja na mradi wa
ujenzi wa njia ya kusambaza umeme kutoka Iringa hadi Shinyanga.
Kati
ya miradi hiyo 16, asilimia 34 ni ya sekta ya ujenzi wa barabara,
asilimia 13 ni ya kilimo, asilimia 12.5 ni ya maji, asilimia 11.2 ni ya
nishati ikifuatiwa na ile sekta za afya, elimu. Sekta nyingine
zinachukua asilimia 18.7 kati ya miradi hiyo.
Miongoni
mwa miradi mikubwa ya barabara ambayo inagharimiwa miongoni mwa miradi
hiyo 16 ni ule wa ujenzi wa barabara ya Iringa-Dodoma yenye kilomita
260 na ule wa ujenzi wa barabara ya Tunduru-Namtumbo yenye kilomita
193.
Wiki
ijayo, miradi ya kufufua ujenzi wa barabara za Dodoma-Babati na
Mangaka-Tunduru iliyocheleweshwa kwa sababu mbali mbali, itawasilishwa
kwenye Bodi ya AfDB.
Mwisho.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
31 Machi, 2012





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)