Rais Jakaya Kikwete Aagana na Mabalozi Wapya wa Tanzania Nchini Italia,Uganda na Msumbiji Ikulu Jijini Dar es Salaam - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Rais Jakaya Kikwete Aagana na Mabalozi Wapya wa Tanzania Nchini Italia,Uganda na Msumbiji Ikulu Jijini Dar es Salaam

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na balozi Mpya wa Tanzania nchini Msumbiji Mhe.Bi Shamim Nyanduga ikulu jijini Dar es Salaam jana.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Balozi mpya wa Tanzania nchini Uganda,Dkt.Ladislaus Komba ikulu jijini Dar es Salaam jana.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete jana ameagana na mabalozi wapya watatu watakaoiwakilisha Tanzania nchi za nje.Mabalozi waliokwenda ikulu kumuaga Rais Kikwete ni pamoja na Dkt.James Msekela anayekwenda Italia, Dkt.Ladislaus Komba anayekwenda Uganda na Mhe.Bi.Shamim Nyanduga anayekwenda Msumbiji.Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Balozi Mpya wa Tanzania nchini Italia Dkt.James Msekela ikulu jijini Dar es Salaam jana.Picha na Freddy Maro-IKULU

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages