Aliyekuwa Katibu Mkuu Msaidizi wa TUSA, Andrea Lesso Hange, enzi za uhai wake.
Ndugu Wanachama, wana michezo na Watanzania kwa Ujumla.
TAARIFA YA MSIBA WA ALIYEKUWA KATIBU MKUU MSAIDIZI MAREHEMU ANDREA HANGE (1970-2012)
Kwa niaba ya Shirikisho la michezo la vyuo Vikuu Tanzania(Tanzania University Sports Association)
Nawataarifu
kuwa tulipokea kwa masikitiko makubwa msiba wa Kiongozi mwenzetu wa
TUSA, Mpendwa wetu Ndg. Andrea Lesso Hange ambaye hadi kifo chake
alikuwa Katibu Mkuu Msaidizi wa TUSA na Mhadhiri Msaidizi wa Chuo Kikuu
cha Dar es Salaam.
Kifo
chake Kilitokea tarehe 02/03/2012 huko Swedeni alikokuwa masomoni.
Taarifa tulizonazo ni kuwa mwili wake ulikutwa chumbani kwake. Uchunguzi
wa kifo chake bado unaendelea.
Taarifa
tulizo nazo kama chama ni kuwa mwili utawasili hapa nchini tarehe
20/03/12 na unatarajiwa kuzikwa tarehe 21/03/12 Kwa hivi sasa Msiba upo
nyumbani kwake Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Karibu na Hall One.
Tunawaomba
wanachama wote wa TUSA, wanafunzi wote waliosoma Elimu kwa michezo
nyakati tofauti pale Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, wanamichezo wote na
watanzania kwa ujumla tukutane wote kwa pamoja tarehe 19/03/12 ili
kufanikisha shughuli hii.
Watu wote tushirikiane katika kipindi hiki kigumu kwani mwili umesubiriwa kwa muda mrefu na gharama zimekuwa kubwa.
Pia unaombwa kutembelea Blog ya TUSA (http://tusadailyblog.blogspot.com/) kwa kupata taarifa nyinginezo kuhusu msiba huu.
Asante Sana kwa Ushiriakiano Wenu
NOEL KIUNSI
KATIBU MKUU TUSA
NOEL B. KIUNSI
PRINCIPAL GAMES TUTOR
UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM
P.O. BOX 35091
DAR ES SALAAM
TANZANIA
+255713263556
KATIBU MKUU TUSA
NOEL B. KIUNSI
PRINCIPAL GAMES TUTOR
UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM
P.O. BOX 35091
DAR ES SALAAM
TANZANIA
+255713263556
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)